HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2017

TANZANIA PRISONS YAIGOMEA YANGA U20 NA KUTWAA KOMBE LA MECHI ZA HISANI 2017 UWANJA WA NYUMBANI


Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania, Godfrey Simbeye, akimkabidhi Kombe, Nahodha wa timu ya Tanzania Prisons, Laurian Mpalile, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga U20 katika mchezo wa Hisani wa fainali wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kulia kwake) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya, (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda. Picha zote na Muhidin Sufiani.
Mshambuliaji wa Yanga U20, Said Mussa (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid.

Mshambuliaji wa Yanga U20, Samwel Geryson (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote.

Beki wa Yanga U20, Mawazo Gawasa (kushoto) akiruka kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid.

Beki wa Yanga U20, Mohamed Nassor (kulia) akipiga krosi huku Salum Bosco wa Tanzania Prisons, akijaribu kuzuia wakati wa mchezo wa Fainali wa Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.

No comments:

Post a Comment

Pages