HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2017

Kikwete awafunda wasanii wa Tanzania

Na Talib Ussi, Zanzibar

Rais Mstaafuwa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewashauri watengenezaji Filamu wa Tanzania kujiendeleza katika kazi yao hiyo ili waweze kuingia katika ushindani wa soko la Dunia.

Kikwete aliyaeleza hayo Zanzibar Juzi Usiku alipozindua Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) ambalo limehudhuriwa na wasanii mbali mbali kutoka Afrika na Dunia kwa Ujumla.

Alisema Wetengenezaji wa Filamu wa Tanzania wasiridhike na walichokipata ni vyema kujiendeleza zaidi wafikie hatua ya kuingia katika ulimwengu wa ushindani.

“Unapoangalia Filamu za wenzetu, halafu ukajaukaangalia za kwetu basi unaweza kuona kuwa sisi bado sana lakini kiasi Fulani tumejitahidi ni vyema tukajiendeleza zaidi” alieleza Kikwete.

Aliewataka Wasanii hao kuongeza elimu ili siku moja waweza kuingia katika Mashindani nan Filamu za Kimataifa ikiwemo Bowlwood na Hollwood.

“Ni ukweli usiopingika sanaa kwetu imetengeneza ajira nyingi mnoo, sasa kama ni hivyo ni vyema kile ambacho tunakizalisha basi kiwe na ubora wenye kuvutia” alieleza Kikwete.

Sambamba na hilo Kikwete alisikitishwa na watunzi wa Filamu wa hapa nchini kutokana na kuyakacha madarasa ya kujiendeleza ambayo yanendeshwa bikla ya malipo.

“Leo ZIFF wameazisha darasa maalumu la kutengeneza Skripti lakini wanaokuja kujifunza woote wanatoka njee hii ni aibu kwa kweli” alifahamisha Kikwete.

Aidha aliwataka Watunzi wa Filamu kutambua kuwa Tamasha la ZIFF ni la kwao hivyo kulitumia kuonesha uwezo wao na upande mwengine njia ya kujifunza.

Katika Tamasha hilo Kikwete alikabidhiwa zawadi maalumu ya mtu maarufu aliyetukuka kutoka kwa wajumbe wa bodi ya tamasha hilo la kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi.-

Kwa upande wake wake Mjumbe wa Bodi ya ZIFF Mahmoud Thabiti Kombo aliwataka Watanzania kulitumia vyema tmasha hilo kwani linafursa nyingi zikiwemo za uchumi na maendeleo.

Alieleza kuwa katika Tamasha hilo la mwaka huu tayari zaidi ya wageni alfu 14 tayari wameingia Zanzibar na kueleza kuwa kila mmoja atafaidika na ugeni huo.

Manega mauzo wa Kampuni ya Internet (Zanlink) Shahzmal Tim ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo aliwaomba makampuni mengine ya ndani kujitokeza zaidi kufadhili tamasha hilo ili liwe bora zaidi kwa maslahin ya taifa.

“Tunapolifanya tamasha hili la ZIFF kuwa bora wageni wengi wataingia nchini na pato la nchi na wanachi litaongezeka” alieleza

Tamasha hilo mwaka huu limetimiza miaka 20 tangu kuazishwa kwake Visiwani Zanzibar ambapo hushirikisha wasanini tofauti duniani.

No comments:

Post a Comment

Pages