HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2017

Mfuko wa PSPF Wakabidhi Mashuka Kwa Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akipokea mashuka kutoka kwa Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Hazina Konde (katikati) na Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi. Faidha Thatau wakikabidhi mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika majengo mapya wa hospitali hiyo Zanzibar. 
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali kwa Wanachama wake Bima ya Afya kwa wateja wao. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akitowa shukrani kwa Uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao huo na kuwataka isiwe mwisho iwe ni endelevu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa hospitali hiyo uwezo ukiruhusu.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar kulia Bi Faidha Khatau akimkabidhi mashuka Afisa Muunguzi katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Bi. Fatma Ali Mzee na kushoto Afisa Mfawidhi Msaidizi Bi Hazina Konde, wakiwa katika moja ya Wodi ya Watoto katika hospitali mpya ya Watoto Mnazi Mmoja. 
Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar.  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

Pages