HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2017

RUSHWA YAMPELEKA JELA MIAKA MITATU ASKARI POLISI

Na Walter Mguluchuma, Katavi
 
ALIYEKUWA askari wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha Konsitebo Peter Kashuta katika Kituo cha Polisi Mwese wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi amenusurika kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kulipa faini mahakamani kiasi cha Sh 500,000-

Hiyo ni baada ya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kumuhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh 500,000/- baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi cha Sh 700,000/-

Akisoma hukumu hiyo hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Mpanda , Chiganga Ntengwa
alieleza kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa upande wa mashataka ambao haukutia shaka kuwa mshtakiwa alikuwa ametenda kosa hilo .

Alisema kuwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa yanakwenda sambamba isipokuwa Mahakam hiyo imetia hatiani kwa kosa la kupokea rushwaambapo upande wa mashtaka uliita mashahidi wan ne.

Akitoa hukumu hiyo , Hakimu Ntengwa alisema kuwa mshtakiwa ametiwa hatiani kwa mujibu wa kifunngu cha Sheria namba 15 cha Sheria ya kupambana na kuzuia rushwa, sura ya 11 ya 2007.

Awali waendesha mashtaka wa Takukuru , Bahati Haule akisaidiwa na Simon Buchwa walidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari , 09 mwaka jana katika kijiji cha Mwese kilichopo katika wilaya ya Tanganyika katika mkoa wa Katavi . 
 
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio , Mshtakiwa aliomba rushwa kiasi cha Sh 700,000/- kutoka kwa Luchega Mambalu ambaye
alikuwa amefunguliwa jarada la kesi katika Kituo cha Polisi Mwese.

Katika utetezi wake Mahakamani hapo mshitakiwa alidai kuwa yeye hakutenda kosa hilo kwani siku hiyo maafisa wa Takukuru hawakumkamata na fedha yoyote ile
 
Madai ambayo yalipingwa vikali na waendesha mashitaka wa Takukuru kwa kile walichodai kuwa kitendo cha mshitakiwa kukimbia na alipokamatwa hakukubali na badala yake alianza kupigana makonde na maafisa fao na kisha aliweza kupufa fedha hizo ambazo zilikuwa ni kielelezo kwenye kesi hiyo ilikuwa ni ushahidi tosha wakumtia hatiani.

Mshitakiwa hata hivyo aliweza kulipa faini ya Tshs 500,000 na kusalimika kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

No comments:

Post a Comment

Pages