HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2017

SPORTPESA YATOA SHUKRANI KWA WANAHABARI, SERIKALI, VYOMBO VYA DOLA NA WANANCHI KUFANIKISHA ZIARA YA EVERTON

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, ambapo alitoa shukrani kwa wanahabari, vyombo vya dola, serikali na watanzania kwa kufanikisha ziara ya timu ya Everton ya Uingereza hapa nchini. (Picha na Richard Mwaikenda).

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Tarimba alisema kuwa ziara ya Everton nchini imekuwa ni ya mafanikio makubwa kimichezo, kiuchumi, kijamii na hasa kuutangaza vilivyo utalii wa Tanzania Duniani.

Tarimba hakusita pia kuishukuru Ikulu kwa kuwapa sapoti kubwa kufanikisha ziara ya Everton hasa katika masuala ya kumpata mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kuruhusu vyombo vya dola kwa ajili ya usalama wa timu hiyo.

"Kwa niaba ya SportPesa ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu hiyo, tutakuwa wachoyo wa fadhila kama tutashindwa kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walituunga mkono katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya ziara hii yanafanikiwa." Alisema Tarimba na kuongeza kuwa...

Napenda Kumshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa baraka zake, lakini pia nipende kumshukuru Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa utayari wa kuwapokea wageni wetu ."
 
Alimshukuru pia Waziri wa Habari, Utamadjuni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya wizara hiyo kwa kuwa bega kwabega katika jukumu hilo hizo. Pia hakusita kutoa pole kwa waziri huyo kwa kufiwa na mkewe.

No comments:

Post a Comment

Pages