HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2017

WASANII WATAKIWA KUTOKATA TAMAA

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wazanzibar wametakiwa kutokata tamaa katika kufanya kazi za usaniii ikiwemo utengenezaji wa filamu kwa kukosa kuona faida mapema.

Hayo yameelezwa Visiwani humu na mjumbe wa bodi wa taasisi ya Zanzibar Emerson Foundation Suleiman Hemed wakati wakizindua utoaji wa Tunzo ya pili ya Emerson kwa vijana wa Kizanzibar ili kuwatia moyo katika utengenezaji wa filamu kuelekea katika Tamasha la kimataifa la Nchi za Jahazi ( ZIFF) ambalo hufanyika Zanzibar.

Alifahamisha kuwa Emerson ambaye alikuwa mtengenezaji filamu wa mwanzo katika Visiwa vya Zanzibar na kuwaomba wasanii wakizanzibar kufuata nyao za msanii huyo ili kufikia malengo waliojiwekea.

“Unaweza kuona wasanii wetu muda mfupi wamekata tama kwa kukosa kuona faida mapema, lakini ni waambie tusikate tama kwani faida haiji mara moja na inataka juhudi tuu na tuwe na moyo wa kujituma tu basi tutaiona faida kubwa” alieleza Hemed.

Alifahamisha kuwa wako baadhi wa watengenezaji wa Filamu ambao wametengeneza filamu zaidi ya kumi bila ya kupata faida lakini hawakukata tama na kudai kuwa leo faida wameiona.

Sambamba na hilo Hemed lieleza kuwa wameazisha tunzo hiyo kwa lengo la kuwahamasisha vijana wa Kizanzibar ili waweze kushiriki kikamilifu katika mashindano ya filamu ili na wao waweze kuwa na filamu bora.

“Tunataka kuona vipaji vya vijana wetu, vinaonekana na kwa kila mzanzibar ambaye atatengeneza Filamu, tunampatia Zawadi kwa lengo la kumpa moyo” alieleza Hemed.

Aidha aliwataka vijana hao wanapotengeneza Filamu, wasitoke kwenye madili ya Kizanzibar na utamaduni wake kwani zinaweza kukosa ubora.

Ali Saleh ambaye ni Mujumbe wa Bido ya Tunzo hiyo na Mbunge wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar alieleza kuwa wameazisha tunzo hiyo ili vijana watengenezaji wa Filamu wa Zanzibar wasiwe watazamaji na badala yake wawe sehemu ya Tamasha hilo.

Tupo kwa ajili ya kuwawezesha vijana wetu kimashindano sio tu kushiriki na mwaka huu wa pili wa tunzo umeonesha mafanikio kutokana kuwepo Filamu nane ambazo zitaoneshwa katika Tamasha la kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF)” alieleza Ali Saleh.

Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi liliaza Jana Jioni Kisiwani Unguja ambapo wasani kutoka nchi mbali mbali wameshiriki.

No comments:

Post a Comment

Pages