HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2017

Wataalam wa APRM Waisifu Serikali ya Rais Magufuli Kiutawala Bora

Na Bushiri Matenda na Immaculate Makilika- MAELEZO

Waatalaam wa Mpango wa Kijitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM) wameelezea kuridhishwana Serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika kusimamia misingi ya Demokrasia na UtawalaBora nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Tathmini za Nchi katika Sekretariati ya APRM na Mratibu wa Mchakato wa Tanzania, Dkt. Rachel Mukamunana alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Slaam wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa ripoti ya APRM utakaofanywa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Rachel alisema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa masuala yanayohusu utawala bora ikiwemo kutatua kero mbalimbali zikiwemo zile zinazohusu masuala ya muungano.

“Serikali ya Rais Magufuli imeonesha kujitoa kwa dhati katika kusimamia masuala ya utawala bora na uzinduzi wa ripoti hii ni kiashara tosha cha dhamira ya serikali katika kusimamia misingi ya utwala bora”, alieleza.

Kutoka na kujitoa huko kwa seriklai, Dkt. Rachel alisema kuwa anatarajia serikali ya Tanzania itaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizoanishwa katika ripoti hiyo ya mwaka 2012 ambayo inayotarajiwa kuzinduliwa kesho (leo).

Nae Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib alieleza kuwa ripoti hiyo imeanisha sifa ambazo Tanzania imekuwa ikisifiwa nazo kuwa ni pamoja na kudumisha amani na umoja, kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50, pamoja na uboreshwaji wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, usawa wa kijinsia na Teknolojia na habari na mawasiliano (TEHAMA).

Alibainisha sifa zingine linazotajwa kwa Tanzania kuwa ni kulinda haki binadamu, matumizi ya lugha moja ya kiswahili, na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini.

Katibu huyo alisema kuwa uzinduzi wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria kimojawapo cha utekelezaji rasmi ya yale yaliyoandikwa kwenye ripoti   pia kielelezo cha utayari wa Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Rehema alisema kuwa lengo la APRM ni kuzisaidia nchi za Kiafrika, Tanzania ikiwa mwanachama mmoja wapo, kuhakikisha kuwa zinaimarisha utawala bora. Hii ni kwa kuwashirikisha wananchi wao kubanisha changamoto ili kuzigeuza kuwa fursa  za maendeleo na mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na  nchi nyingine.

APRM Tanzania ilipewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia majukumu ya nchi katika kuratibu tathimini ya Utawala bora kwa mujibu wa wa miongozi ya Wakuu wa Nchi za Kiafrika.

No comments:

Post a Comment

Pages