HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2017

WAZIRI MKUU NA MSHINDI WA TUZO YA UINGEREZA

Samuel Mwanyika (19) akiwa ameshika tuzo wakati anatambulishwa kwa Wabunge mjini Dodoma. Samuel alishinda tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingereza bada ya kutuma picha ya pundamilia wawili wakiota jua kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Watoto kutoka nchi 18 walishiriki shindano la picha kwa mwaka 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samuel Mwanyika, mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Katikati ni Mama wa mtoto huyoSophie Mshangama (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel Mwanyika aliyeshinda tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa Juni 8, 2017 na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Katikati ni Mama wa mtoto huyo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingerezakwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Pages