HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2017

JUVICUF Walia na Ajira

Na Talib Ussi, Zanzibar

Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) imeeleza kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana limekuwa sugu na linasababisha athari kubwa kwa vijana waliowengi nchini Tanzania kwa madai kuwa Serikali zoote mbiliu zimekosa mipango dhidi ya yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Habari wa Jumuiya ya Vijana chama hicho JUVICUF Abeid Khamis Bakar kupitia taarifa kwa vyombo vya habari
Alifahamisha kwamba  tatizo ambalo limezidi kutokana na mwenendo wa serikali mpya chini ya Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kushindwa kuweka mikakati ya kuwaajiri vijana na badala yake kuwanyanyasa wale ambao wamejiajiri.

 Alieleza kuwa vijana wengi wamesambaa mitaani bila ya kazi ya kufanya licha ya kuwa na sifa ya kuajiriwa lakini alidai kuwa Serikali hizo zinaonyesha hazina malengo mazuri kwa vijana wa Nchii.

alifahamisha kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ( SMZ), tatizo ni kubwa zaidi,kwa maelezo kuwa tangu  kuingia madarakani kwa njia isiyokuwa ya kidemokrasia, serikali ya Dk. Ali Muhammed Shein haijatangaza ajira toshelezi (hajafikia hata thumni ya mahitaji ya ajira kwa vijana) pamoja na ukweli kwamba wapo vijana wengi walioomba nafasi za kazi maeneo tofauti kama vile katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na hadi kufanya usaili miezi kadhaa lakini hakuna jibu lolooote walilopewa hadi leo.

“Wanajigamba wanaserikali lakini vijana wao hawana ajira hata hawashughuliki, tujiulizeni walichaguliwa kweli na wananchi hawa” aliuliza mkurugenzi huyo wa habari JUVICUF.

alisema kuwa wanapata imani kuwa SMZ haina uwezo wa kutoa ajira kwa vijana hasa kwa kuzingatia kwa madai kuwa  hivi karibuni kulitangazwa nafasi za ajira katika Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Zanzibar, na vijana zaidi 100 kutoka Unguja nan Pemba  na wakati nafasi zinazotakiwa ni mbili tu na hadi leo hakuitwa mtu.

“ Hii ina maana mahitaji ya ajira ni makubwa zaidi ya uwezo wa serikali. Zanzibar kuna malalamiko ya mwenendo usiofaa wa serikali na taasisi zake kutoa fursa za ajira kwa upendeleo unaozingatia misingi ya kiitikadi (mirengo ya kisiasa). Hili ni tatizo kubwa kama lilivyo la kuzuia fursa za kupanda daraja na kujiendeleza kielimu kwa wafanyakazi waliopo serikalini” alieleza.

JUVICUF Taifa kwa kuyaona hayo na mengine mengi, imewaomba vijana popote walipo katika nchi yao, kutovunjika moyo kwa mwenendo wa mfumo unaowakwamisha katika fikra za kimaendeleo. 

Aidha  imewataka vijana wote nchini  washikamane kwa kuwa kitu kimoja katika kukemea uzuiaji wa haki zao unaofanywa na Serikali au kikundi chochote kile na waendelee kuamini kuwa kufikiri na hatimaye kuamua kwa ajili ya maslahi yao ya kimaendeleo, ni haki yao isiyonyang’anyika kwa mujibu wa katiba.

Alieleza kuwa inafaa kukemewa kwa namna yoyote ile na inapotokea wanapaswa kushikamana na kuipigania kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kikatiba zilizopo.

“Ndipo watakapojihakikishia mustakbali wao kuhusu maendeleo ya kiuchumi, kielimu, kisiasa na kiutamaduni” alieleza Bakar.

No comments:

Post a Comment

Pages