HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2017

TIGO KUTOA SMARTPHONE ZENYE MUDA WA BURE WA MAONGEZI KILA SAA KWA SAA 24

 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni mpya ya Jaza Ujazwe ambapo simu za kisasa 720 zitatolewa kila siku kwa washindi wa promosheni hiyo. Kulia ni  Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akionesha moja ya simu aina ya Teco S1 zitakazotolewa katika promosheni hiyo.
Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma, akizungumzia promosheni hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo  Tanzania, bado inawavutia wateja wake tena na prmosheni kubwa ambayo itashuhudia wateja hao  wakiondoka na simu za mkononi za kisasa (Smartphones) kila saa kwa saa 24 kila siku. Simu za mkononi zitatolewa zikiwa na muda wa  bure wa  mawasiliano kwa mwaka mmoja.

 Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za kisasa (Smartphones) 720  zipo tayari kuchukuliwa katika kampeni ya promosheni hii mpya.  Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa tu kwa kuzijaza simu zao muda wa maongezi  kwa kukwangua kadi, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo kwa ajili ya kushinda  moja ya Smartphones za Tecno S1 ambayo itakuwa tayari kuchukuliwa  kila saa,  kila siku, katika siku saba za wiki.
                                             
Tofauti na promosheni nyingine ambapo ni wateja wachache tu wanapata zawadi chache, promosheni hii ya Tigo imethibitisha kusimama mahali ambapo  kila mteja mmoja anazawadiwa  kila anapojaza. Washindi wa Smartphone ya Tecno S1  watafurahia mawasiliano ya bure kwa mwaka mmoja ambapo zawadi nyingine za kushinda zinajumuisha bonasi ya bure katika  sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno ( SMS) kulingana na muundo wa matumizi wa wateja.

Akitangaza zawadi hizo mpya, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa kampuni hiyo kwa mara nyingine tena imefurahishwa na mwitiko chanya wa wateja kwa kampeni maarufu ya  Jaza Ujazwe na ndiyo sababu imewafanya waongeze zawadi za kuvutia zaidi pamoja na bonasi zaidi za kusisimua kama ishara ya shukrani.
  
"Ni sehemu ya utamaduni wa Tigo katika  kutambua kuungwa mkono kusiko na ukomo ambao wateja wetu wametupa. Ndiyo maana, tunaamini kwamba wanastahili kupewa shukrani  kwa kujitoa kwao kwa kwa ajili ya  bidhaa  na huduma zetu. Tuna furaha  mara nyingine tena, kuwapatia  wateja wetu zawadi hizi, zitakazowawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu za maisha ya kidijitali ", alisema Mpinga.


Tuzo za kusisimua zinaendana na  kuongezeka kwa miundombinu ya mtandao wa kisasa ya Tigo, aliongeza Mpinga akibainisha kuwa kipaumbele muhimu cha kampuni kilikuwa kikizingatia mahitaji ya wateja na kutoa suluhisho linalofaa kushughulikia mahitaji hayo.

 "Wateja wote wa Tigo wanastahili kupokea tuzo; tunatarajia kukidhi mahitaji ya mteja ya kuwa na uzoefu usio na  dosari kila wakati wanapowasiliana kwa chapa zetu.

Tunaamini kuwa wateja wetu watafurahishwa na zawadi hizi  mpya ikiwa ni pamoja na bonasi kwa dakika, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data wanazozawadiwa na hivyo  kuimarisha utamaduni wao wa mawasiliano, "alibainisha Mpinga.

No comments:

Post a Comment

Pages