Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

Kaimu Mkurugenzi wa JNIA akutana na wadau

 Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (katikati) akimsikiliza kwa makini bw. Is’haq Al.zadjali wa Shirika la ndege la Oman katika mkutano alioitisha kujadili masuala mbalimbali na wahusika wa mashirika hayo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JNIA TBII leo.
 Wadau mbalimbali wa mashirika ya ndege yanayofanya kazi kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakiandika mambo mbalimbali yaliyokuwa yakisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka alipokutana nao leo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TBII.
Bw. Iqbal Sajan wa shirika la ndege la Auric (aliyesisimama) akichangia hoja kwenye mkutano wa mashirika ya ndege ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka wa kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha huduma.

Kaimu Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Rose Commino (wa kwanza kushoto) akiwafafanulia masuala mbalimbali wafanyakazi wa mashirika ya ndege zinazofanya safari zake JNIA, katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi, Bw. Johannes Munanka (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment