HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2017

KAMANDA MUSILIMU AIPONGEZA PUMA ENERGY KWA KUWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOCHORA PICHA BORA ZA ATHARI ZA USALAMA BARABARANI

Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Mwanafunzi Nasri Mwema akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano hayo
Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani.

Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa sh. mil. 2.
Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo.
Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao.

No comments:

Post a Comment

Pages