HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 21, 2017

MHESHIMIWA KUBENEA AFIKISHWA MBELE YA KAMATI

Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeahirisha kumuhoji Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe. Saed Kubenea kutokana na kufika mbele ya Kamati hiyo akiwa mgonjwa.

Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati majira ya saa 4 asubuhi akiwa katika baiskeli ya wagonjwa ya miguu minne (Wheel chair) chini ya ulinzi wa Askarii wa Jeshi la polisi.

Akizungumzia katika kiao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika alisema kamati hiyo imekutana kutokana na kuletewa shauri na Mhe. Spika la kumuita Mbunge huyo kwa madai ya kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli alizozitoa katika kanisa moja Jijini Dar es Salaam.

 “Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inakutana pale inapoletewa shauri na Mhe. Spika, tumeletwa mashauri ya Mhe. Kubenea, ya kudharau Mamlaka ya Spika kwa kauli ambazo amezitoa katika kanisa la huko Dar Es Salaam,” alisema.

Alisema taratibu zinamtaka mtu anayetakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kupelekewa Hati ya kuitwa na kwamba alishapelekewa.


Alisema hata hivyo Mhe. Kubenea amepelekwa akiwa katika baiskeli ya wagonjwa na kuiomba Kamati impangie siku nyingine na kwamba Kamati hiyo imeridhia ombi lake.

“Kamati baada ya kumsikliza Mhe. Kubenea imeridhia ombi lake la kumpangia tarehe nyingine kwa kumpa muda wa kuangalia afya yake mpaka atakapopona,”
 alisema.

Mhe. Mkuchika aliagizaa Mhe. Kubenea apelekwe katika Zahanati ya Bunge ili aweze kupewa huduma ya kwanza.

Awali Mhe. Kubenea baada ya kuhojiwa na kamati kama ataweza kuzungumza katika kikao hicho aliiomba kamati kumpangia siku nyingine kwa kuwa asingeweza kuzungumza kwa wakati ule kutokana na kuwa katika maumivu makali.

Septemba 12, mwaka huu, Mhe. Spika Job Ndugai aliagiza Mbunge huyo kufika mbele ya kamati hiyo kwa kuhojiwa kuhusiana na tuhuma alizozitoa wakati wa Ibada tarehe 10 Septemba, 2017 kwamba Mhe. Spika alisema uongo Bungeni wakati akitangaza idadi ya risasi zilizopigwa kwenye gari la Mhe. Tundu  Lissu.

Mhe. Spika pia aliiagiza Kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe kufuatia kauli zake alizozitoa kwenye mitandao kwamba Mhimili wa Bunge umewekwa mfukoni na Serikali na kwamba Bunge lilikosea kushughulikia Taarifa za Kamati kuhusu Almasi na Tanzanite.

No comments:

Post a Comment

Pages