HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2017

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2017, kuhusu zoezi la kuwakamata wafanyabiashara wanaouza CD feki za wasanii pamoja na wale wanaotumia kompyuta kuingiza nyimbo za wasanii katika simu, zoezi hilo litafanyika nchi nzima.

DAR ES SALAAM, Tanzania
Baada ya Kampuni ya Udalali ya Msama kupata mafanikio katika zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki za Kazi za wasanii jjini Dar es Salaam kampuni hiyo imepanga kuanza zoezi hilo nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa Sh. Mil. 10 ili kusaidia juhudi za kampuni yake katika kupambana na watu wanaojishughulisha na wizi wa kazi za wasanii.

Msama amemshukuru Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kwa kutambua mchango wake hivyo atahakikisha anaongeza juhudi katika kuhakikisha kazi za wasanii zinalindwa ili waweze kunufaika na kazi zao.

“Wale wanaofanya biashara ya wizi wa kazi za wasanii waache na watafute kazi nyingine za kufanya kwani zoezi hili si kwa mkoa wa Dar es Salaam tu ni zoezi la nchi nzima na lazima watu wajifunze kulipa kodi kwani pesa za kodi zinaleta maendeleo katika nchi yetu.”

Msama amesema kuwa zoezi hilo litakuwa la aina yake kwani wataingia katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam ili kuwasambaratisha wafanyabiashara haramu wa kazi za wasanii ambao wamekuwa wakinufaika na kuwaacha wasanii wakiwa katika hali duni.

Tutaingia katika vichochoro vvyote vya mkoa wa Dar es Salaam hasa katika maeneo yaliyokithiri kwa biashara hiyo yakiwemo Ubungo, Kimara, Manzese, Kariakoo, Mbagala, Temeke, Kigamboni kabla ya kuhamia mikoani.

“Huu ni wakati kwa wasanii kunufaika na kazi zao na tutahakikisha tutafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi na
hii yote ni kwa kujali kazi za wasanii”alisema Msama.

Aidha Msama aliwaomba wananchi kununua kazi za wasanii zenye stika halali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuhakikisha hakuna wizi wowote unaotokea katika kazi mbalimbali za wasanii.

No comments:

Post a Comment

Pages