HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 14, 2017

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB PAMOJA NA WATEJA WACHANGIA MILIONI 15 UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, wakati alipowasili Makao Makuu ya Benki ya CRDB kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa zoezi la ukusanyaji fedha kwa ajili ujenzi wa ofisi za walimu mkoani Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akionyesha sehemu ya michango ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala, Beatus Segeja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la ukusanyaji fedha kwa ajili ujenzi wa ofisi za walimu mkoani Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la ukusanyaji fedha kwa ajili ujenzi wa ofisi za walimu Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaaam, Paul Makonda (akikata utepe/kuweka fedha) kwenye boksi maalum kuashiria kuzindua rasmi zoezi la ukusanyaji fedha kwa ajili ujenzi wa ofisi za walimu mkoani Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo Mheshimiwa Makonda pia alipokea kiasi cha shilingi milioni 18 kilichochangwa na wafanyakazi na wateja wa benki hiyo. *kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi za ofisi za walimu Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza Solomon Urio.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akitoa mchango wa Sh. 400,000 katika boksi maalum lililopo katika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Ofisi za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchangia.

Makamu Mwenyekiti Kamati ya Ujenzi Ofisi za Walimu, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akichangia ujenzi wa ofisi za walimu.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wa Kati wa Benki ya CRDB, Jesca Nyachiro, akichangia ujenzi wa ofisi za walimu.

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa, akichangia.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisaini kitabu cha wageni alipofika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe.

Wakionyesha furaha.

Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.

Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, namna ya kutumia huduma ya SimBanking.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Freddy Nshekanabo, akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwa kuwezesha zoezi la uchangiaji kufanyika kwa umakini.


Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (katikati), akifuatilia hafla ya uzinduzi wa uchangiaji ofisi za walimu Mkoa wa Dar es Salaam.

Tully Mwambapa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

Sehemu ya michango ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na wateja wa benki hiyo.


Dar es Salaam Tanzania, Novemba 14, 2017


Wafanyakazi na wateja wa Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Dokta Charles Kimei leo wamekabidhi msaada wa shilingi milioni 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda, ili kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule za msingi na sekondari mkoani humo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mchango huo na kuzindua rasmi zoezi la hilo la uchangiaji iliyofanyika katika Makao makuu ya Benki hiyo jijini la Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dokta Charles Kimei alisema msaada huo unatokana na michango ya wafanyakazi na wateja wa Benki ambao wamehamasika katika kuisaidia serikali kutatua changamoto ya upungufu wa ofisi za walimu jijini humo. “Hii ni sehemu tu ya michango inayoendelea kukusanywa na wafanyakazi wa benki ya CRDB kupitia matawi yake yote 252 nchini. Fedha zinazokabidhiwa leo ni za kutoka Makao Makuu na tawi moja la Azikiwe jijini Dar es Salaam” alisema Dokta Kimei.
“Wakati tukikabidhi mchango wetu wa shilingi milioni 100 mimi na timu yangu ya Benki ya CRDB, tulikuahidi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa tutaendelea kuhamasisha uchangiaji huu wa ujenzi wa ofisi za walimu kupitia matawi yetu ili kuwapa fursa wafanyakazi na wateja wetu kutoa mchango yao ya hali na mali ili kufanikisha zoezi hili” alisema Dokta Kimei.
Dokta Kimei alisema katika kuhakikisha wanatekeleza adhma hiyo, Benki ya CRDB ilitengeneza masandaku maalumu ya kuchangisha fedha “donation boxes” ambayo yalisambazwa katika idara na matawi yote ya Benki hiyo Tanzania nzima.

Dokta Kimei aliongeza kuwa katika kipindi kifupi cha miezi miezi miwili tu, kiasi cha shilingi milioni 15 kilikusanywa kutoka Makao Makuu na tawi kubwa la Azikiwe lilipo jijini humo, hivyo kuonyesha uhamasikaji wa hali ya juu wa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo kwenye kuchangia maendeleo ya mkoa wao na taifa zima kwa ujumla wake.
“Leo tunakabidhi sehemu tu ya michango hiyo kwani jijini Dar es Salaam bado tuna matawi mengine 20 ambayo yanaendelea na zoezi hili la ukusanyaji.

Tutakapokuwa tayari tutawasilisha tena kwako Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa. Nina furaha kusema kuwa mwamko umekuwa mzuri kwani wafanyakazi na wateja wetu wengi wameonyesha kuguswa na jitihada za serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini na hii ndio sababu kubwa iliyochangia kukusanya kiasi hiki cha pesa”, alisema Dokta Kimei.

Dokta Kimei alisema ili kuendelea na utekelezaji wa sera ya Benki hiyo ya kuisaidia jamii “Corporate Social Responsibilty”, Menejimenti ya Benki ya CRDB imekubaliana kuendelea na zoezi hilo la uhamasishaji wa kuchangia ujenzi wa ofisi za walimu hadi mwezi Desemba mwaka huu.

“Dhumuni letu ni kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki katika uchangiaji huu, pia tumekubaliana kusambaza maboksi yetu ya kukusanyia michango kwenye matawi yote nchi nzima, ili kusaidia kukusanya michango kwa eneo husika”, alisema Dokta Kimei.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliushukuru uongozi wa Benki ya CRDB kwa kuonyesha uzalendo wa hali juu na kuwezesha kupatikana kwa msaada huo ambao ni michango ya wafanyakazi na wateja wa Benki ya CRDB.
“Naomba niipongeze Benki ya CRDB kwa ubunifu huu wa hali ya juu ama hakika hii ni Benki ya kizalendo na siku zote imekuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine hapa nchini.

Dokta Kimei alipoahidi kuwa ataweka miundo mbinu itakayowezesha wafanyakazi na wateja wa Benki ya CRDB kupata fursa ya kuchangia, sikuwa na hakika kama mwamko utakuwa mkubwa hivi. Lakini michango hii tunayopokea leo ni kielelezo tosha cha uzalendo wa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam katika kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo. Asanteni sana Benki ya CRDB”, alisema Mheshimiwa Paul Makonda.

Benki ya CRDB ndio ilikuwa taasisi ya kwanza kuunga mkono juhudi za serikali ya mkoa wa Dar es Salaam katika ujenzi wa ofisi za walimu ambapo ilitoa msaada wa shilingi milioni 200 ambazo zitataolewa kwa mikupuo miwili. Shilingi milioni mia moja zilizotolewa awali ziliweza kufanikisha ununuzi wa jumla ya mifuko 10,000 ya saruji ambayo itasaidia kujenga jumla ya vyumba 40 vya ofisi za walimu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Akimalizia hotuba yake, Mheshimiwa Makonda aliwasihi wadau wengine kuendelea kuchangia zoezi hilo kupitia akaunti maalum ya uchangiaji wa ujenzi wa ofisi hizo yenye nambari “0150296180200” iliyopo katika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages