Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

MUAROBAINI WA KUKOSEKANA UZAZI HUU HAPA

NA SHEHE SEMTAWA

KLINIKI ya Matumaini Heberisti imewataka wanandoa wanaosumbuliwa na tatizo la uzazi waache kusononeka, baadala yake wafike katika kituo hicho ili aweze kupatiwa tiba ya kumaliza tatizo hilo.

Mmiliki wa kituo hicho, Tausi Kagunduka,  aliyasema hayo baada ya kubaini kuwa wapo wanandoa wengi ambao wameigia katika migogoro ya kifamilia kutokana na kukosa watoto kwa muda mrefu tangu walipofunga ndoa.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam leo,Tausi alisema Kiliniki hiyo imejipanga kusaidia baadhi ya wanandoa wanaokabiliwa na tatizo hilo, ambalo kwa sasa anaamini linaweza kutibika.

Alisema, ameweka wazi kuwa tatizo hilo linaweza kutoweka kwa wanandoa endapo watatumia dawa ya Engelo ambayo ilivumbuliwa na kliniki hiyo na kuthibitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto miaka sita iliyopita.

"Dawa hiyo pamoja na milinolino zilithibitishwa kwa kumbukumbu Namba 341/VOLXIII/11/40 na Namba TBB/SLM.II/KNG.II pamoja na LAB No.341/2011, hata hivyo kwa kila hatua tunayofanya tunawasiliana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali.

"Mimi nashauri mwenye tatizo hilo aje au ni vema wahusika wakafika kwenye kliniki yetu pamoja ili wote waweze kupata tiba, tunafanya hivyo kwa sababu tatizo hilo linaweza kujitokeza kwa yeyote kati yao bila kujijua,"alisema Tausi.

Tausi, alisema licha ya kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo upungufu wa kinga mwilini, lakini amebaini kuwa wagonjwa wengi wanaojitokeza katika kliniki hiyo ni wanawake wanaokabiliwa na tatizo la uzazi.

"Unajua mafanikio katika tiba hiyo yatasaidia kuimarisha ndoa za watu kwani kuna baadhi ya ndoa zilivunjika kutokana na kukosa watoto, kwa hiyo nawaomba wafike Buguruni Marapa karibu na kanisa la mabati na kisha wanipigie simu namba 0717303050 na 0784624554,"alifafanua Tausi. 

Akizungumzia kuhusu dawa ya mlinolino, Tausi, alidai dawa hiyo inatibu maradhi mbalimbali ikiwemo upungufu wa kinga mwilini.

Alidai kuwa tangu wagonjwa wake walipoanza kuitumia dawa hiyo,  kwenda kupimwa hospitalini baadhi yao yawalidai kwamba waligundulika kuwa wamepona.

"Tangu nimeanza dawa ya mlinolino kutibu watu wenye upungufu wa kinga mwilini sijapata msukosuko wowote kutoka serikalini kwani baada ya kuwapatia matibabu hayo nawashauri waende Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kuona kama wamepona au la,"alisema Tausi.

Aidha, Tausi alisema Kliniki hiyo pia imekuwa ikitoa msaada wa matibabu bure kwa watoto ambao wazazi wao wamefariki kutokana na maradhi ya ukimwi.

Aliongeza kuwa gharama za matibabu hayo kwa watu wazima ni sh.200,000 huku akibainisha kuwa waliweka bei hiyo ili kila mwenye tatizo hilo aweze kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment