HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2017

Msimu wa pili ‘Ishi Kistaa’ wazinduliwa

Na Mwandishi Wetu

MSIMU mpya wa shoo ya Ishi kistaa umezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam ambapo wasanii wa bongo fleva na bongo movie watapata fursa ya kukutana na mashabiki wao na kubadilishana mawazo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mratibu wa Ishi Kistaa, Beatrice Mbwiga kutoka kampuni ya Greentelecom, alisema kuwa katika msimu huu wa pili mambo yameongezwa ili kuwafanya wasanii na mashabiki wake kufurahia mambo mbalimbali.

“Kwa msimu huu wa pili tofauti na msimu wa kwanza, mambo mengi yameongezwa, wasanii wa ndani wanaweza wakaunganishwa na wasanii wakubwa nje ya Tanzania ambao wanawakubali, lakini pia mashabiki watakaokuwa wakifuatilia wanaweza wakashinda zawadi mbalimbali,” alisema Beatrice.

Alisema kuwa kwa mashabiki watakaoufuatilia Ishi Kistaa kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye namba 15670 wanaweza wakashinda zawadi mbalimbali kama simu, safari ya nje ya nchi pamoja na vocha za manunuzi.

“Lakini pia watapata nafasi ya kukutana na wasanii wao wanaowapenda na kubadilishana nao mawazo,” aliongezea kusema Beatrice.

Kwa upande wake, msanii wa bongo fleva, Barnaba ambaye alishiriki Ishi Kistaa msimu wa kwanza, alisema kupitia ishi kistaa wasanii wanaweza wakafaidika na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kujitanua kimataifa.

“Unapata nafasi ya kuuza nyimbo zako kimtandao, lakini pia unajiingizia fedha kwa kuwa sehemu ya ishi kistaa,” alisema Barnaba.
Msanii wa Bongo Fleva, Elias Barnabas, akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa shindano la Ishi Kistaa linalodhaminiwa na Kampuni ya Greentelcom. Kushoto ni Meneja Mradi wa Green Telecom, Beatrice Felix.
 Msanii wa Bongo Fleva, Msami Jiovan Msamibaby, akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa shindano la Ishi Kistaa. Katikati ni Meneja Mradi wa Green Telecom, Beatrice Felix.
 Meneja Mradi wa Green Telecom, Beatrice Felix, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa shindano la Ishi Kista. Kulia ni msanii wa Bongo Fleva, Elias Barnabas, kushoto Msanii wa Bongo Fleva, Msami Jiovan Msamibaby.

No comments:

Post a Comment

Pages