Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

Ujenzi barabara sita Kimara, Kibaha kuanza mwishoni mwa Desemba

NA SULEIMAN MSUYA

SERIKALI imesema ujenzi wa barabara ya njia sita yenye urefu wa kilomita 16 kutoka Kimara Ubungo hadi Kibaha mkoani Pwani utaanza mwishoni mwa mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara ya kukagua ubomoji wa jengo la Shirika la Umeme Tanzania na maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo ya Kimara hadi Kibaha.

Mbarawa alisema serikali imedhamiria kuboresha miundombinu yote nchini hivyo ujenzi huo wa barabara ya njia nne utaondoa kero ya foleni katika barabara ya Morogoro.

Alisema serikali inatambua adha walizopata wananchi na kuwa haikuwa na lengo baya tofauti na kuleta maendeleo.

"Mwisho wa mwezi huu ujenzi wa njia mbili kila upande kutoka Kimara hadi Kibaha utaanza ni matumaini yetu ujenzi ukikamilika utapunguza foleni ya kuingia jijini," alisema.

Mbarawa alisema pamoja na ujenzi wa barabara hiyo serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kurahisisha huduma ya usafiri nchini.

Waziri Mbarawa aliwataka wananchi waliokandokando na barabara kuacha kujenga katika hifadhi ya barabara kwani serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria.

"Sheria ipo wazi tangu mwaka 1932 wakati wa mkoloni inataja upana wa bararaba ni mita 120 kila upande hivyo naomba msivunje ndio sheria yetu," alisema.

Alisema katika kuonesha mfano serikali imevunja ofisi sake hivyo ni dhahiri hakuna atakayeonewa huruma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale alisema ofisi yake imepeleka wahandisi wa kufanya tathmini na upembuzi yakinifu hivyo mkandarasi ataanza ujenzi mwishoni mwa mwaka.

Alisema wanataka barabara hizo zijengwe kwa haraka ili kupunguza adha ya foleni iliyopo sasa wakati wa kuingia mjini.

"Ujenzi huu utakuwa wa aina yake mkandarasi anachora michoro anajenga hakuna kusubiri hapa kazi tu," alisema.

Mhandisi Mfugale alisema Tanroads imejipanga kikamilifu kuhakikisha miundombinu inakuwa bora ili iweze kupitika kipindi chote cha mwaka.

No comments:

Post a Comment