NA JANETH JOVIN
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January
Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuchukua hatua
za haraka katika kukabiliana na tatizo la mafuriko na uharibifu wa
mazingira katika jiji hilo.
Mama Samia amewataka viongozi hao kuunda kamati maalum ya kushughulikia matatizo hayo haraka iwezekanavyo.
Makamu ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati
akiongoza mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu changamoto ya mafuriko na
hifadhi ya mazingira katika jiji hilo.
Alisema kwa muda mrefu kumekuwa hakuna umakini katika kusimamia masuala ya mazingira nchini licha kuwepo kwa sheria mbalimbali.
"Mambo mengi na hasara zinazotekea wakati wa mafuriko
zinasababishwa na sisi wenyewe watu wamekuwa hawana utamaduni wa
kuyatunza mazingira yao sasa natoa maagizo hiundwe kamati ya mazingira
haraka ambayo itapokea miradi yote ya kila wilaya na kuangalia ipi
itatekelezeka.
Kamati hii itakaoundwa haina haja ya fedha na nisije
nikasikia kuwa imeshindwa kufanya kazi kutokana na kukosa na fedha kwani
ni sehemu ya majukumu yao ya kazi"alisema
Aidha alisema kuna uhitaji wa kutolewa elimu ya mazingira kwa jamii na kupeana taarifa mbalimbali zinazohusiana na mazingira.
Naye Waziri Makamba alisema ni wakati wa kutafakari na
kupata jawabu la kudumu la suala la mafuriko yanayotokea katika jiji la
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment