HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 16, 2018

Mkutano Mkuu wa 13 wa TAGCO kufanyika Arusha machi 12-16 jijini Arusha


Mweyekiti wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarjiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 Machi Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mwenezi wa TAGCO Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus na Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi na Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete

Kaimu Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akisistiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO, Abdul Njaidi, Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus. Picha na MELEZO
..............................................................................

Na Florah Raphael-Fullshangwe-Dar es Salaam

Mkutano Mkuu wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo , unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12-16 Machi mwaka huu mkoani Arusha ambapo jumla ya maofisa 300 wanatarajiwa kishiriki katika mkutano huo.

Akiongea Na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama hicho Paschal Shelutete amesema kuwa lengo kuu kuelekea mkutano huo ni kukumbushana wajibu na majukumu yao serikalini.

Aidha amesema kuwa kikao hicho kina kazi ya kuwajengea washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za serikali na kuhakikisha idara ya mawasikiano na uhusiano serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Pia ameongeza na kusema kuwa katika mkutano huo jumla ya mada 14 zitaongelewa ambazo zitajikita zaidi kwenye masuala mbalimbali yahusuyo habari, mawasiliano na itifaki.

Pia amesema kuwa mada hizo zitawasilishwa na wataalam watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano na kuongeza kuwa kutakuwepo mijadala na fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya maaafisa mawasiliano na wadau wengine wa habari.

Mwisho kabisa amewaasa Maafisa Uabari, mawasiliano, uhusiano na Itifaki kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 7 machi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages