HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 08, 2018

Tigo Yawazawadia Mamilionea Wapya


Wateja watatu wa Tigo Pesa wapokea TZS 15 milioni, 10 millioni na 5 milioni kila mmoja.
  • 12 wengine washinda TZS milioni moja (1) na wengine 49 wapata TSH 500,000 kila mmoja katika kilele cha promosheni

Dar es Salaam, 5 Januari, 2018. 



Tigo Tanzania, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, leo imegeuza Watanzania watatu (3) kuwa mamilionea kupitia promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’ iliyofikia tamati usiku wa mkesha wa mwaka mpya.



Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, Dar es Salaam leo amepokea donge nono la shilingi 15 milioni kutoka Tigo.  ‘Sasa nina rasilimali itakayoniwezesha kufanikisha malengo yangu ya kufanya kilimo mwaka huu,’ alisema.



Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma naye alishinda shilingi milioni kumi (10) baada ya kutumia huduma ya Tigo Pesa katika kipindi cha msimu wa sikukuu na mwaka mpya. ‘Nilikuwa nimeshalala wakati nilipokea simu kutoka Tigo iliyonifahamisha kuwa nimeshinda mamilioni ya shilingi. Nilidhani kuwa ni ndoto na asubuhi nilipoamka nikawapigia Tigo simu kuhakikisha taarifa hizi na kugundua kuwa ni za kweli. Nimeanza mwaka mpya kwa nguvu mpya!’ alisema.



Naye Mariam Josef Maligisa kutoka Nagangu mkoani Lindi alisema kuwa maisha yake kama mkulima na mfanya biashara ndogo yataboreshwa kwa kiasi kikubwa na zawadi ya shilingi milioni tano (5) kutoka Tigo. ‘Sikuwa na nyenzo za kilimo ila sasa nitaweza kuongeza eneo ninalolima pamoja na kukuza biashara yangu,’ aliongeza.



Washindi wengine 12 walinyakua zawadi za shilingi milioni moja (1) kila mmoja huku wengine 49 wakijipatia zawadi za shilingi laki tano (500,000/-) kila mmoja kama zawadi za kila siku.



Akikabidhi zawadi kwa washindi katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alielezea furaha yake kuwa promosheni hiyo imefanikiwa kuboresha maisha ya wateja wa Tigo Pesa.



  ‘Tumefikia lengo kuu la promosheni hii ambalo lilikuwa ni kufanikisha ndoto za wateja wetu katika kipindi cha sikukuu na mwaka mpya. 



Alibainisha kuwa katika promosheni hiyo, Tigo imetoa jumla ya TZS 120 milioni kama zawadi kwa washindi 153 tofauti kutoka maeneo tofauti ya nchi, ambapo wateja walipata fursa ya kushinda baada ya kufanya miamala kupitia Tigo Pesa katika kipindi cha sikukuu na mwaka mpya.



‘Pia tunajivunia mchango wetu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu wote nchini. Tigo Pesa inawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma, kupokea na kufanya miamala ya fedha inayofikia zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi. Huu ni mchango mkubwa kwa uchumi wa watu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea fedha. Ni sehemu ya maisha,’ aliongeza.



Tigo Pesa ndio huduma ya pili kwa ukubwa nchini ya huduma za pesa kwa njia ya simu za mkononi, inayojivunia mtandao mpana wa mawakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.



Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.


Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini.  Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.
Mshindi wa wa Shs. Milioni 5 wa promosheni ya Tumia Tigo upate nafasi ya kushinda, Mariam Josef Maligisa kutoka Nagangu mkoani Lindi, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi zao.

No comments:

Post a Comment

Pages