HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2018

MAKAMU WA RAIS AKAGUA UJENZI WA UKUTA WA FUKWE YA KIGAMBONI

Makamu wa Rais (katikati) Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya ujenzi wa ukuta wa Kigamboni kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd, Premji Pindoria (kushoto) kulia NIU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Poul Makonda. (Picha na Janeth Jovin).

NA JANETH JOVIN

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuyatunza mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na athari za  mabadiliko ya tabianchi.

Mama Samia amesema kama jamii haitaweza kufanya hivyo basi hupo uwezekano mkubwa katika maeneo ya nchi hasa kwenye fukwe za Bahari ardhi yake kumomonyoka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa ukuta katika fukwe ya Kigamboni na Ocean Road, Samia alisema kwa sasa mazingira yameanza kuharibiwa nchini hivyo ni muhimu kuchukua hatua ya kuzuia yale yote yanayosababisha uharibifu huo.

Alisema ni lazima kila mtu kuwa rafiki wa mazingira kwa kuacha kukata miti hovyo na kutochimba mchanga baharini na kwenye vyanzo vya maji.

"Suala la mazingira ni letu sote na tukumbuke kuwa unapoharibu mazingira lazima yatakuja kukuadhibu baadae hivyo niwaombe wananchi wayatunze ili yatutunze na tuweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, "alisema.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba alisema mradi huo wa ukuta ni miongoni mwa miradi mbalimbali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 93 utazuia kubomoka kwa chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

"Nchi yetu inaufukwe wa bahari upatao Kilomita 1400, eneo hili ni kubwa na athari zilizopo huko kutokana na watu kutotunza mazingira ni kubwa mno hivyo ni muhimu kuendelea kupaza sauti na kukemea uharibifu wa mazingira, " alisema.

Naye Meneja mradi huo Fred Manyika alisema urefu wa ukuta uliyojengwa kigamboni ni Mita 500 na wa Ocean Road ni mita 920.

No comments:

Post a Comment

Pages