Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

BENKI YA CRDB YAZINDUA KADI ZA MIKOPO

NA MWANDISHI WETU
 
BENKI ya CRDB imeanzisha mfumo wa kadi za mikopo bila riba kwa wateja wake ili kuwapa wigo mpana wa manunuzi popote walipo.
 
Mfumo huo umefanywa kwa ushirikiano na Taasisi ya Kimataifa ya Mastecard ambapo kadi aina mbili zitakuwa na viwango tofauti vya mikopo na muda wa marejesho.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alizitaja kadi hizo kuwa ni TemboCard World Rewards na TemboCard Gold Credit-Card.
 
“Hii Tembocard World Rewards ni maalum kwa wateja wakubwa ambapo mteja ataweza kukopa hadi Sh. milioni 50 kwa wakati mmoja na muda wa kurudisha ni siku 50.

“…Mteja wa Tembocard Gold Credit Card ni yule wa kati na wajasiriamali ambapo watapata mkopo hadi wa hadi Sh. milioni 20 atakaolazimika kuurudisha ndani ya siku 45.
 
“Anayerudisha kwa wakati hatozwi riba lakini ukishindwa kurejesha kwa muda huo utatozwa asilimia tano ya fedha hizo kama riba, tunaamini mikopo hiyo isiyo na masharti itasisimua uchumi wa nchi,” alisisitiza Dk. Kimei.
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mteja atakayekopa au kumiliki kadi hiyo atapata punguzo la bei kwenye maduka, hoteli za kifahari na migahawa popote waendapo duniani iwapo watafanya malipo kwa kadi hiyo.
 
Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wateja wa CRDB na watanzania kutembelea matawi ya benki hhiyo ili kujaza fomu za maombi ya kupata kadi hizo za mikopo ambazo zinapatikana pia kwenye tovuti ya benki.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kadi za malipo za Tembocard World Reward Credit Card na Tembocard Gold Credit Card uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kadi za malipo za Tembocard World Reward Credit Card na Tembocard Gold Credit Card uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Mwambapa.
Baadhi ya Wakurigenzi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa kadi za malipo za Tembocard World Reward Credit Card na Tembocard Gold Credit Card uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei.

No comments:

Post a Comment