HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2018

DC MGANDILWA AMTAKA MKANDARASI WA MAJI KUKAMILISHA MRADI HARAKA

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji katika Kata ya Kisarawe II. 

Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba, wamepitia maeneo mbalimbali ambayo vituo vya kutolea maji vilipo na kushuhudia baadhi vikitoa maji na baadhi vikiwa havitoi maji. 

DC Mgandilwa amemtaka mkandarasi anayejenga mradi huo kuhakikisha anarekebisha maeneo ambayo yana itilafu ili maji yaweze kutoka katika vituo vyote na kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa mitaa husika. 

DC Mgandilwa ameongeza kuwa, Kama mkandarasi atashindwa kumalizia mradi huo kwa wakati na kwa kiwango kinachostahili kwa kisingizio kuwa pesa ilitumika yote wajiandae kuirudisha pesa hiyo haraka ili ifanye kazi iliyokusudiwa kwani pesa iliyotolewa ilikuwa inatosha kabisa kumaliza mradi huo vinginevyo watakuwa waliitumia vibaya. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni amesema kuwa mradi huo aliupokea kutoka katika manispaa ya Temeke ukiwa katika hali ambayo sio nzuri na umekuwa ukiendelea kusuasua licha ya kuufatilia mara kwa mara .

Ameongeza kuwa kwa sasa anasubiria mkandarasi huyo amalizie mradi ukaguliwe ili kujiridhisha na alete madai ya pesa ambayo atakuwa anadai alipwe kwani serikali inataka wananchi wapate maji haraka.

No comments:

Post a Comment

Pages