HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2018

HALMASHAURI YA GEITA YAPEWA GARI LA CHANJO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi mbunge wa jimbo la Geita, Joseph Musukuma gari aina Tunland Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.

Amemkabidhi gari hilo leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo,  Bw. Ali Kidwaka na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Bw. Elisha Lupuga.

Waziri Mkuu amesema amekabidhi gari hilo ili kuiwezesha Halmashauri hiyo kuboresha huduma za chanjo pamoja na za mama na mtoto kwa sababu suala la usafiri lilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaikabili wilaya hiyo.

“Mbunge alinieleza matatizo mbalimbali yanayoikabili Halmashauri ya wilaya ya Geita, ambayo ni pamoja na gari la kutolea huduma mbalimbali, hivyo leo namkabidhi gari hili ili likahudumie wananchi katika sekta ya afya”.

Kwa upande wake, Bw. Musukuma alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita. Alisema gari hilo ni zuri sana na watalitumia kama ilivyokusudiwa.

“Haya ndio matunda ya Serikali ya Awamu ya Tano. Naishukuru sana Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali wilayani Geita zikiwemo za afya na maji.”

Amesema atahakikisha gari hilo linatunzwa na linatumika kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa ambayo ni huduma za chanjo pamoja na huduma za mama na mtoto.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 22, 2018.

No comments:

Post a Comment

Pages