HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 19, 2018

PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na  uongozi wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu, wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ya barabara mkoani humo. Wa Kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe.
 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98, mkoani Simiyu. Ujenzi huo umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46.
 Gari maalum likimwaga lami ya mwisho katika barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3, wilayani Maswa, Mkoani Simiyu. Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 61.46.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe kuhusu umuhimu wa kutunza barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Simiyu,
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3, wilayani humo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Kushoto ni Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu. 
 Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

Pages