Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

MAUAJI YA KATIBU WA CHADEMA WAZIRI MWIGULU AMUAGIZA IGP KUCHUNGUZA TUKIO HILO

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Daniel John ambaye alikiwa ni katibu wa Chadema kata ya hananasif  yaliyotokea kinondoni  jijini Dar es salaam.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani kagera wilaya ya muleba katika kata ya kasindaga wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa mkoani humo

Waziri Dr Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili. Alisema Waziri Mwigulu

Ameongeza kusema kuwa maswala ya demkrasia huamuliwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki na kila mkutu anayo haki ya kuwa katika chama chochote cha siasa nchini.

Naye mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenarali mstaafu Salum Kijuu amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote ndani ya mkoa huo kuhakikisha zoezi la kuandikisha vitambukisho vya Taifa linakwenda vizuri na kwakuzingatia sheria bila rushwa na upendeleo wowote.

Amewataka wananchi wajitokeze katika utambuzi wa watu kwani mkoa huo unauingiliano wa watu kutoka nchi jirani za burundi,Rwanda na uganda hivyo inaweza kuwa rahisi kwao kujiandikisha na kupata kitambukisho hicho.

No comments:

Post a Comment