Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

MAZISHI YA TAMBWE KATIKA PICHA

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, akitoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Kada na Kiongozi wa chama hicho, Richard Tambwe Hiza nyumbani kwa marehemu, Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam, Februari 10 2018.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vicent Mashinji, akitoa salamu za rambirambi wakati wa ibada ya kuaga mwili wa kada wa chama hicho, Richard Tambwe Hiza, nyumbani kwake Mbagala jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiwaongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye ibada ya mazishi ya kada na kiongozi wa chama hicho, Richard Tambwe Hiza, kuaga mwili wake.
Walinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Red Briged), wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa kada wa Chama hicho, Richard Tambwe Hiza kuelekea katika Makaburi ya Chang'ombe.
Mariam Tambwe, ambaye ni mke wa marehemu Tambwe Hiza, akiweka udongo katika kaburi la mumewe wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Changómbe jijini Dar es Salaam.

Jeneza lililokuwa na mwili wa Richard Tambwe Hiza, likishushwa kaburini.

No comments:

Post a Comment