HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2018

Meya wa Jiji la Dar aungana na wananchi kupima magonjwa ya Kisukari na Presha

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameungana na wakazi wa jijini hapa katika kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania kilichopo jijini hapa.

Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.

Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

"Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu, angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila mwananchi anahitaji kuipata" amesema Meya Mwita.

Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao. Imetolewa leo Februali 11 na Christina Mwagala Afisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji.

No comments:

Post a Comment

Pages