HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2018

TIGO YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA NYAKANYAKA

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto), akimkabidhi zawadi ya simu  aina ya Tecno R6, Mariam Saleh, aliyoshinda katika promosheni ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Februari 16. (Picha na Francis Dande). 
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea. 


NA MWANDISHI WETU

WASHINDI 36 wa shindano la Nyakanyaka, jana wamekabidhiwa zawadi za simu za mkononi baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano lililofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salam, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, alisema wametoa zawadi hizo katika wiki ya pili ya shindano.

Alisema washindi zaidi ya 1000 wanatarajiwa kupatikana katika shindano hilo ambalo litamalizika baada ya miezi mitatu.

Alisema walianzisha shindano hilo ili kuwashukuru wateja wao kwa kuwa nao katika kipindi chote na linafanyika nchi nzima.

“Tumechezesha droo ya pili ya shindano la Nyakanyaka na kupata washindi 36 ambao tumewapatia zawadi zao, lengo la shindano hili ni kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi katika muda wote,” alisema Woinde.

Aliwataja baadhi ya washindi kuwa ni pamoja na Ibrahim Mohamed, Said Hamza, Emmanuel Adolf, Frank Castory, Sharif Katongoro, William Kupaka, Stela Samweli, Elayan Mtani, Tito Martin, Ramadhan Mbahe na Mariam Saleh.

No comments:

Post a Comment

Pages