HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 22, 2018

TNBC YAISAINI MKATABA WA UBORESHAJI MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI (LIC)

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi na Kiongozi wa Mradi wa LIC, Flemming Winther Olsen wakiweka saini ya mkataba wa kazi wa uboreshaji mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Mikataba hiyo imesainiwa Mei 22, 2018 katika Ofisi za TNBC jijini Dar es Salaam.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi (kushoto), na Kiongozi wa Mradi wa LIC, Flemming Winther Olsen wakibadilishana mkataba baada ya kusaini makubaliano ya kazi baina yao  katika Ofisi za TNBC Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2018.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi, akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa kazi na mradi wa uboreshaji mazingira ya biashara na uwekezaji nchini  (LIC) unaofadhiliwa na Denmark. Kulia ni Kiongozi wa Mradi wa LIC, Flemming Winther Oslen. Kiongozi wa Mradi wa LIC, Flemming Winther Oslen, akiwaelezea waandishi wa habari dhumuni la ufadhili wa mradi huu kwa TNBC ni kutaka kuiinua sekta binafsi na kuipa nguvu na kuweza kushirikiana na serikali katika kuinua uchumi wa nchi. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa TNBC Raymond Mbilinyi.  Imetolewa na Ofisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages