HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2018

KAMPENI YA FURAHA YANGU KATIKA MAANDALIZI YA UPIMAJI VVU

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akiwa ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge (kushoto),  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Prof Faustin Kamuzora (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS  Dk Leonard Maboko (kulia) wakijadili jambo wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi leo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kulia) akipokea maelezo kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi leo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa kwanza kulia) akikagua mabanda ambayo yatatumiwa na wananchi kupima VVU  katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Mhe Mhagama alikuwa ameandamana na kamati ya maadalizi wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge,  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Prof Faustin Kamuzora pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS  Dk Leonard Maboko.

No comments:

Post a Comment

Pages