HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 10, 2018

NMB yajitosa kudhamini Tuzo za Tanzania Top 100

Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kutangaza udhamini wa Tuzo za Tanzania Top 100 wenye thamani ya dola za Marekani 50,000.
Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko Azam Media, Abdul Mohamed, akizungumza katika uzinduzi huo.

Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), akisaini mkataba wa kudhamini  tuzo za Kampuni Bora 100 ‘Tanzania Top 100 Mid-Sized Companies Awards,’ wenye thamani ya dola za Marekani 50,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu.
Kubadilishana hati.
Kuonyesha.

Na Mwandishi Wetu



MSIMU wa nane wa Tuzo za Wafanyabiashara/Kampuni 100 Bora nchini ‘Tanzania Top 100 Mid-Sized Companies Awards,’ umezinduliwa jijini Dar es Salaam, huku Benki ya NMB ikisaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya dola za Marekani 50,000.


Uzinduzi huo ulifanyika jana, ambako mwakilishi wa Kampuni ya KPMG, inayoratibu tuzo hizo, Ketan Shah, alisema pamoja na mambo mengine, Tuzo za Kampuni 100 Bora, zinalenga ya kutambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara nchini.

Shah alisema wanafurahi kuona Benki ya NMB ikikubali kudhamini tuzo hizo, ambazo hutumika kuwapa wafanyabiashara, wajasiriamali na makampuni, mbinu za mafanikio kutoka kwa waliofanikiwa zaifdi, ikiwa ni pamoja na kuonyesha njia za kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Alizitaja miongoni mwa sifa kuu za kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na Kampuni ama mfanyabiashara kuwa na pato linaloanzia Sh. Bilioni 1 hadi 20 kwa mwaka na kuwa na hati safi za ukaguzi wa mahesabu ya kampuni kwa miaka mitatu iliyopita.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, alisema benki yake ina furaha kuwa sehemu ya shindano hilo, linaloratibiwa na KPMG, aliowataja kama wabobezi katika masuala ya utaalamu na ushauri chanya wa kibiashara.

Aliongeza ya kwamba, kwa miaka nane, KPMG imekuwa ikiratibu kwa mafanikio tuzo hizo, ambako wamekuwa wakifanya uchunguzi wa huduma mbalimbali za kibiashara na kuchangia ustawi, maendeleo na mafanikio ya kampuni shiriki na taifa kwa ujumla.

“Leo hii NMB tunapiga hatua kubwa zaidi kwa kuingia ubia na KPMG, ambao wanatarajia kufanya utafiti yakinifu na wa kina, ili kuwapata wafanyabiashara 100 bora nchini. Tunaamini kupitia mchakato huu itatoa fursa kwa washiriki hao kunufaika na huduma zetu,” alisema.

Ukiondoa NMB, wadhamini wenza wa tuzo hizo, ambazo pia hufanyika katika nchi za Kenya na Rwanda kwa miaka 10 sasa, ni pamoja na Kampuni ya Azam Media Ltd, Mwananchi Communication Ltd, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Hyatty Regency.

No comments:

Post a Comment

Pages