HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2018

ALLY HAPI AWATAKA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA KUJITATHIMINI

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema amewataka wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa kujitathimini juu ya utendaji wao.
Amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na na utendaji mbovu wa baadhi ya wafanyakazi wakiwemo wauguzi. 

Amesema hayo wakati akiongea na wakuu wa Idara  a wafanyakazi wa Wilaya hiyo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha Wilaya humo.

Amesema kuna baadhi ya watumishi kufanyakazi kwa mazoea hali inayoshusha uwajibikaji wao kwa Wananchi.
Aidha, ameagiza kuwepo na utaratibu wa kugauwa bure vitambulisho vitakavyowawezesha wazee kupatiwa matibabu bure.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa,  Ally Hapi, akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wilaya ya Iringa juzi. (Picha na Datus Mahendeka-OUT).


No comments:

Post a Comment

Pages