HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2018

Waziri Ummy avipongeza viwanja vya Ndege kwa kudhibiti Ebola

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (watatu kulia) leo akiongoza Matembezi ya Hiyari kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mohamed Kambi.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakipiga picha mbele ya bango lenye ujumbe kuhusiana na ugonjwa wa Ebola la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyofanyika leo kwa kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Kariamjee jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela akiongea na wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa kuanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Viwanja vya Karimjee.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa udhibiti wa ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, baada ya kufanya Matembezi ya Hiyari yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu leo akitembea mbele ya bango la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakati wa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

No comments:

Post a Comment

Pages