HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 14, 2018

DKT. MWANJELWA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE ILI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA UMMA

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko, akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi, mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti  ofisini kwake  jijini  Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na mmoja wa watumishi  wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti  ofisini kwake  jijini  Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

Dodoma, Tanzania
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) ameahidi kushirikiana na watumishi wa ofisi yake kupanga mikakati endelevu itakayowezesha kutoa huduma bora kwa umma na kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa na mtazamo chanya katika kuwahudumia wananchi.
Dkt. Mwanjelwa ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Dkt. Mwanjelwa ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wa ofisi yake kwani kila mtumishi ana mchango na umuhimu wake katika kuboresha utuoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya utumishi na utawala bora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018 na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 14 NOVEMBA, 2018

No comments:

Post a Comment

Pages