HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2018

MSD YABORESHA UPATIKANAJI DAWA JIMBO LA WAZIRI MKUU RUANGWA MKOANI LINDI


 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mahela Njile, akizungumza  na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD), juzi (hawapo pichani), ambao walikuwa wilayani humo kwa ziara ya siku moja ya kutembelea wateja wao na kujua changamoto zao.
 Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Noel Likango (katikati), akizungumza na waandishi wa habari na maofisa wa MSD wakati akiwakaribisha baada ya kufika kwenye hospitali hiyo.
 Duka la Dawa la MSD lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
 Mkazi wa Kilimahewa mjini Ruangwa, Gelard Alila, akizungumzia upatikaji wa dawa.
 Mkazi wa eneo la Mbambabay mjini Ruangwa, Fatma Mpokwe, akitoa shukurani zake kwa serikali kwa kuboresha upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Ruangwa.
 Ofisa  Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akimuelekeza jambo Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Said Mbaruku, kabla ya kuzungumza na wanahabari.
 Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Said Mbaruku, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mifuko maalumu yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito ilivyo ondoa changamoto ya kupata vifaa hivyo kwa walengwa.
Gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.

Na Dotto Mwaibale, Ruangwa Lindi

BOHARI ya Dawa (MSD), imeboresha upatikaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo ni Jimbo la Uchaguzi la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ambapo sasa dawa zinapatikana kwa asilimia 94 ukilinganisha na miaka mitano ya nyuma.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Mahela Njile wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD), juzi ambao walikuwa wilayani humo kwa ziara ya siku moja ya kutembelea wateja wao na kujua changamoto zao.

"Tunaishukuru sasa MSD kwa kuboresha upatikanaji wa dawa katika wilaya yetu tumefikia asilimia 94 kutoka asilimia 70 tuliyo kuwa nayo miaka ya nyuma" alisema Dkt. Njile.

Alisema hali hiyo imetokana na serikali kutenga bajeti kubwa ya fedha katika sekta ya afya na ushirikiano uliopo baina ya hospitali hiyo pamoja na MSD kwani mawasiliano yamekuwa makubwa  na kuwa pale wanapotoa oda ya kuhitaji dawa wamekuwa wakipelekewa kwa wakati na MSD.

"Kwa kusema kweli kama leo hii ningekutana na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurian Rugambwa Bwanakunu ningempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya na ningemwambia asirudi nyuma bali aongeze juhudi zaidi ili kasi yake ya utendaji wa kazi iwe mara dufu ya hapo kwani kazi yake inaonekana na ni ya kiwango cha juu" alisema Njile.

Dkt. Njile aliipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuijali sekta ya afya hasa katika upatikaji wa dawa kila kona ya nchi hii.


Mkazi wa Kitongoji cha Kilimahewa kilichopo mjini Ruangwa, Gelard Alila alisema tangu aanze kutibiwa katika zahanati ya wilaya hiyo kuanzia miaka minne hali ya upatikaji wa dawa ni mzuri na hata zikiwa hazipo kwenye stoo ya hospitali zinapatikana kwenye duka la MSD lililopo hospitali hapo.

"Sasa hivi hakika serikali imeboresha sekta ya afya dawa tunazipata na kama zikiwa hazipo kule kwenye dirisha la hospitali tunanunua kwenye duka la MSD ingawa changamoto kubwa ni kwa wagonjwa wenye Bima ya Afya tujengewe mazingira yakupa dawa duka la MSD kwa kukatwa malipo kupitia bima yetu badala ya kutoa fedha taslimu" alisema Alila. 

Mkazi mwingine wa Kitongoji cha Mbambabay, Fatma Mpokwa alimpongeza Rais John Magufuli,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine kwa kuboresha upatikaji wa dawa katika Zahanati, Vituo vya afya na Hospitali ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo palikuwa na changamoto kubwa.

Muuguzi wa Hospitali hiyo, Saida Mbaruku alisema mifuko maalumu yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito inawasaidia sana wakina mama kwani zamani walikuwa wakishindwa kupata vifaa hivyo kwa pamoja na kujikuta wakiwa na changamoto lakini sasa hivi kila anapokuwa akienda kliniki anauwezo wa kulipia kwa awamu na anapokaribia kujifungua anakuwa amekamisha kulipia vifaa vyote na kukabidhiwa mfuko wake.

MSD ilifanya ziara ya kutembelea wateja wao  Mkoa wa Mtwara ili kujua changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi ambapo ilitembelea Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Minyembe, Kituo cha Afya cha Likombe, Mkutimango, Mkwedu, Mnali na Hospitali ya Wilaya ya Masasi Mkomaindo, Zahanati ya Mkuti na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa iliyopo mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment

Pages