HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2018

Tigo yaja na programu ya Tigo Kinara kwa ajili ya wateja wake


NA MWANDISHI WETU 

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua programu mpya inayojulikana kama Tigo Kinara inayowapa wateja faida mbali mbali ikiwemo dakika za kupiga simu za kimataifa, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na vifurushi vya intaneti katika kifurushi kimoja.

Kupitia program ya Tigo Kinara wanaweza kupata manufaa zaidi kama vile kuokoa salio lililobaki na usafiri wa bure wa Uber jijini Dar es Salaam.

 ‘’Ikiwa ni sehemu ya azma yetu kutoa huduma za kiwango cha kimataifa zinazojali mahitaji ya kipekee ya wateja wetu muhimu, Tigo Kinara ni huduma inayowapa wateja manufaa ya kimaisha na kuwawezesha kufurahia matumizi ya simu pamoja na ofa murwa kwa huduma na bidhaa mbalimbali. Tigo Kinara pia ni programu inayotoa manufaa ya kipekee kutoka kwa kampuni na watoa huduma washirika,’ Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema. 

Kwa mujibu wa Tarik, Tigo Kinara inawaruhusu wateja kufurahia huduma za kidigitali kwa kiwango cha kimataifa  kwenye mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+. “Ubunifu huu unadhihirisha kuwa Tigo ndio mtandao unaobuni bidhaa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wateja kwa sababu Kinara ni suluhisho la mambo ya msingi kwa mahitaji tofauti,” anasema.

 ‘Kifurushi cha Kinara kinawawezesha ateja kuokoa au kujumuisha salio ambalo hawajalitumia katika vifurushi vyao kila mara wanapojiunga na vifurushi vipya vya wiki au mwezi. Tigo Kinara pia inakupa fursa ya kufurahia punguzo kabambe unapotumia usafiri wa Uber ndani ya jiji la Dar Salaam,’ Boudiaf naongeza.

Kinara pia inazo faida zinazojumuisha huduma maalum unapopiga simu kwa kitengo cha Huduma kwa Wateja ama unapotembelea maduka ya Tigo; pamoja na programu za kusisimua za Tigo Pesa kupitia mtandao mpana zaidi wa wafanya biashara nchini Tanzania. Vile vile wateja wanapokea manufaa zaidi ya hadi miezi sita ya intaneti bure na punguzo la bei kila wanaponunua simu janja na ving’amuzi vya mtandao kutoka Tigo.

Kinara ni mahususi zaidi kwa wateja wanaofanya matumizi makubwa ya intaneti, SMS au huduma za sauti kwa kuwapa huduma kamili za Tigo ndani ya kifurushi kimoja.

No comments:

Post a Comment

Pages