HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2018

Waziri Mwakyembe kufikisha Changamoto za Veta kwa viongozi Husika

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Tamasha la Michezo na Maonesho  ya Vyuo vya Ufundi yaliyozinduliwa leo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha Veta Kanda ya Kati mara baada ya uzinduzi wa tamasha la michezo na maonyesho ya vyuo vya ufundi yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu, Anthony Mavunde. (Picha na Maelezo).

Na Anitha Jonas – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi viongozi wa Veta kufikisha vilio  vya changamoto zao kwa viongozi husika.
Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo leo jijijni Dodoma  alipokuwa akizindua Tamasha la Michezo na Maonesho ya  vyuo vya ufundi Kanda ya Kati Dodoma,mara baada ya viongozi hao kusoma risala yao kuhusu tamasha lao ambalo litadumu kwa wiki nzima  lengo likiwa ni  kujenga umoja na kuboresha mahusiano kwa vyuo  vya ufundi pamoja na kuweka mikakati ya kutoa elimu bora yenye kusaidia taifa kufika malengo ya uchumi wa Kati na nchi ya viwanda.
“Kwanza ninawapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kuwajenga vijana wenye ujuzi ambao wanaelewa thamani ya michezo kwani michezo ni afya na michezo ni  ajira kwa hakika jambo hili mlilolifanya ni jambo  zuri na pia natoa rai kwenu wanamichezo wote mnaoshiriki michezo hii kucheza kwa amani ,“alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo Mhe.Mwakyembe alisisitiza kuwa katika mashindano hayo asingependa kusikia kuwepo kwa wachezaji mamluki ambao siyo wanamichezo kutoka katika vyuo husika vilivyoshiriki tamasha hilo.
Pamoja na hayo nae Naibu Waziri Ofisi ya Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde alieleza mipango mbalimbali serikali iliyojiwekea ya  kushirikiana na VETA kwa ajili ya kuhakikisha inawasaidia vijana  kupata mafunzo ya ufundi ambayo yatawawezesha kujiajiri na kufanikisha adhima ya nchi yetu kufikia uchumi wakati na nchi ya Viwanda.
“Kupitia umoja huu wa vyuo vya ufundi kwa kanda ya kati waliyouanzisha nitajitahidi kuwasimamia na kuhakikisha wanaanzisha kiwanda chao wenyewe cha mfano ,“Mhe.Mavunde.
Aidha,nae Kaimu Mkuu wa Chuo Veta Kanda ya Kati Bw.Ramadhan Mataka alieleza kuwa VETA kama wasimamizi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi nchini hivi karibuni uongozi wa Kanda ya Kati imevifungia vyuo ishirini vilivyokuwa havina viwango vya kutoa mafunzo kukuzingatia sheria na utaratibu wa hadhi ya vyuo vya ufundi.
 “Kupitia Umoja wa Vyuo vya Ufundi tunataka tuunde mkakati madhubuti wa kuboresha kozi zetu na kuhakikisha tunatoa mafunzo yenye ubora  ambayo yatatusaidia wote kutembea katika njia moja kwa manufaa ya taifa letu na uchumi wa nchi  yetu,”Bw.Mataka.
Sambamba na hayo  Bw. Mataka alitoa rai kwa vyuo vyote vya ufundi vilivyopo Kanda ya Kati ambavyo havijasajiliwa vijisajili haraka ili kurasimisha shughuli zao,”Bw.Mataka
Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyuo vya Ufundi Dodoma, Bw.Jeremia  Philip alieleza kuwa umoja huo unamalengo mbalimbali ikiwemo kuboresha masomo ya mafunzo ya ufundi na kuwaongezea vijana ujasiri wa kujiajiri mara baada ya kufuzu masomo yao.
 Pamoja na hayo Bw.Jeremia alieleza kuwa umoja huo umeanzisha mpango wa kurudisha darasani vijana ambao hawakupata elimu waliyochini ya miaka kumi na tano wa kuwapeleka darasani  na kuwapatia mafunzo ya ufundi kwa lengo la kuwasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Pages