HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 16, 2018

Benjamin Michael ang'ara mbio za Ngorongoro

 Wanariadha wakipita katika moja ya barabara ya Arusha wakichuana katika mbio za kilometa 10 wakati wa mashindano ya taifa ya wazi ya Ngorongoro jana. (Na Mpigapicha Wetu).
 Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 100 wakati wa mashindano ya wazi ya taifa ya riadha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
  Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 5,000 za wakati wa mashindano ya wazi ya taifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mwanariadha Fabiani Sule wa Jeshi la Polisi akimaliza namba moja katika mbio za mita 5000.

 Wanariadha wa mbi za mita 5000 wakiwa katika picha ya pamoja.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Gidabuday akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Ramadhani Ng'anzi.
 
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MASHINDANO ya wazi ya taifa ya riadha yamefanyika jijini Arusha na kushuhudiwa na watazamaji kibao waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Tofauti na mashindano hayo yanapofanyikia jijini Dar es Salaam, uwanja huo ulikuwa na watazamaji kibao walioshuhudia wanariadha wengi wa mkoa mwenyeji wakitamba katika mbio mbalimbali.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa mara ya kwanza katika mashindano ya taifa yalishirikisha mbio za barabarani za kilometa 10 badala ya zile za uwanjani za meta 10,000, ambazo  jana hazikuwepo.
Katika mbio za kilometa 10, Jackson Mwakombe alimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 32:00.22, baada ya kuongoza kwa muda mrefu mbio hizo akiwaacha wenzake mbali.
Arusha pia ilitwaa medali ya dhahabu katika kilometa 10 kwa wanawake wakati Neema Kisuda alipomaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 40:01.04 akifuatiwa na wanariadha wengine wa Arusha, ambao ni Gloria Makula na Sarah Hiti waliomaliza katika nafasi ya pili na tatu kwa dakika 40:27.98 na 41:26.91.
Benjamin Michael alimaliza wa kwanza kwa kutumia sekunde 10:99, huku Laurent Masatu na Bakari Barnabasi wote wa Arusha wakimaliza katika nafsi ya pili na tatu kwa kutumia sekunde 11:10 na 11:18.
Katika mbio za meta 800, Mariam Salim, Grace Jackson na Shamin Ramadhani wote wa Arusha walimaliza kwa dakika 2:18.09, 2:20.72 na 2:21.87 na kushika nafasi ya kwanza, ya pili na tatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kwa upande wa meta 5,000 wanawake, Arusha ilishika nafasi mbili za kwanza pale, Natalia Elisante na Angelina Daniel walimaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 16:54.52 na 17:18.80 huku Angelina John wa Singida akimaliza wa tatu kwa kutumia dakika 18:10.68.
Katika mbio za meta 800 kwa wanaume, mwanariadha wa Manyara Gabriel Geay alitamba baada ya kumaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 1:50.75 huku akifuatiwa na Faraja Damas na Simon Francis wote wa Arusha waliotumia muda wa dakika 1:52.28 na 1:52.68.
Washindi wa kwanza katika kila mchezo wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, waliondoka na Sh 150,000 kila mmoja wakati wale walioshika nafasi za pili kila mmoja alipata 100,000 na watatu Sh 50,000.

No comments:

Post a Comment

Pages