HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 11, 2018

Kampeni ya 'Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja' inanufaisha vijana Tanzania








Mwandishi Wetu

KAMPENI ya  'Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja' (Each One Teach One) imeanzishwa na  Mfuko wa UBA (UBA Foundation) ikilenga kuwafanya wafanyakazi wa ALLUBA kupata fursa ya kurudisha kwa jamii walichonayo kwa njia zao wenyewe.

Jitihada hizo zimelenga kuwasaidia vijana kupata ujuzi ambao unaweza kuwasaidia kujitengeneza kipato (fedha) kwasiku za mbele.

UBA Tanzania kupitia Mfuko wa UBA imeshiriki katika kampeni ya Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja kwa vijana wa Afrika. 

Kupitia kampeni ya Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja  wafanyakazi wa UBA wanaojitolea wamekuwa wakitumia muda wao kwenda katika jamii kufundisha vijana shughuli mbalimbali kama vile lugha za kigeni, kupigapicha, kubuni mitindo, sanaa ya mapigano, muziki na nyingine.

UBA si kwamba ina mtazamo wa kutoa mafunzo kwa vijana wa Dar es Salaam na Dodoma tu, lakini ina mipango ya kuongeza programu katika maeneo mengine ya nchi.
UBA imekuwepo nchini kwa miaka tisa sasa na imekuwa ikiitikia vizuri wajibu wake kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages