HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2018

MRADI WA ASDIT WATOA MAFUNZO VIONGOZI WA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA WAJUMBE WA KAMATI ZA AFYAWA HALMASHAURI NNE ZA MKOA WA MOROGORO

Dkt. Godfrey Mteyi akitoa elimu kwa viongozi wa afya kutoka vituo 15 vya afya na zahanati 5 katika halmashauri nne za mkoa wa Morogoro kwenye mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa hospitali ya st, Francis halmashauri ya mji mdogo Ifakara kuhusu kuimarisha uongozi na menejimenti kwa watumishi wa afya ikiwemo mfumo wa uongozi, menejimenti,utawala na uwajibikaji, miundombinu na vifaatiba.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob akitoa wito kwa watumishi wa afya katika mafunzo ya kuwajengea uwezo dhidi uongozi na utawala yaliyofanyika katika hospitali ya St, Francis Halmshauri ya mji mdogo wa Ifakara kufanya kazi kwa kufata utaratibu uliopo wa mfumo wa matibabu ili kuondokana na changamoto ya takwimu za wagonjwa na idadi ya dawa na vifaa tiba.
Mtafiti Kiongozi wa Mradi wa kutoa Huduma ya Uzazi Salama kwa mama wajawazito na watoto wachanga (ASIDT) Dk. Angelo Nyamtema, akilezea malengo ya mafunzo ya uongozi na utawala kwa waganga wa afya walioshiriki mafunzo hayo katika hospital ya St, Francis halmashauri ya mji mdogo wa Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Mganga mfawidhi zahanati ya Mlilingwa Morogoro vijijini Winifrida Mayunga akiwasilisha majibu ya mambo ya kufanya kwa haraka inapotokea dharura kutokana na majukumu ya viongozi , anayefata kushoto ni Mratibu wa mradi ASIDT Zabroni Abel Akiandika majibu anayowasilisha mganga mfawidhi wa zahanati ya Mlilingwa.
Watumishi wa afya ambao pia ni viongozi katika halmashauri ya Morogoro vijijini wakijadiliana namna ya kufanya endapo wamekabiliwa na kazi nyingi kwa wakati mmoja ili kuondokana na changamoto ya kukwama kwa huduma pale ambapo wanahitajika. mfano, wakijikita katika uchambuzi wa kipi wakifanye ,kipi wakiache, kipi wakikaimishe na kipi kifanyike baadae . Wa kwanza kulia ni (Grace Massawe muuguzi mkuu wa mkoa wa Morogoro ameshika karamu akielezea mambo ya kuzingatia).  

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Morogoro

Imeelezwa kuwa Mapungufu yanayosababishwa na kutokuwa na ujuzi wa utawala kwa wakuu wa vituo vya afya na zahanati imekuwa ikichangia katika utendaji kazi wa wataalamu haokuwa chini ya kiwango na wakati mwingine kupoteza takwimu halisi za maswala ya wagonjwa .

Akiongea na viongozi wa vituo vya afya, zahanati na wajumbe wa kamati za afya katika halmshauri 4 za mkoani Morogoro wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika uongozi na utawala bora , Mganga mkuu wa Mkoa Morogoro Dkt, Frank Jacob amesema kuwa watumishi wa afya wamekuwa wakipoteza takwimu halisi kutokana na kufanya kazi pasipo kufata vigezo vya utoaji wa huduma hali ambayo inachangiwa na usimamizi usio kuwa thabiti

Mtafiti kiongozi wa mradi wa ASDIT Dkt,Angelo Nyamtema amesema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo ili kuboresha utendaji kazi wa wataalamu hao ambao wakati mwingine unakuwa chini wa kiwango hivyo kukubushwa majukumu yao kama inavyofanyika katika mafunzo haya.

Nyamtema amesema mafunzo hayo yatasaidia kwa kiwango kikubwa uendaji kazi kutokana na wakuu wa vituo na wajumbe wa kamati za afya kupewa madaraka bila kupata mafunzo ya uongozi na utawala.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamekili uwepo wa mapungufu katika swala la takwimu na utendaji katika maeneo yao ya kazi kutokana na watoa huduma wenyewe kutofata utaratibu na wamepongeza hatua ya mradi huo wa ASDIT kutoa mafunzo hayo ambayo yamewakumbusha majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Pages