HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 05, 2018

WASHINDI WA DROO YA PILI YA PROMOSHENI YA JIDABO NA I&M BANK WATANGAZWA

Mteja wa Benki ya I&MBank akichukua kishina wakati wa kumtafuta mmoja kati ya washindi watano promosheni ya ‘JIDABO na I&M Bank,’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo na kulia ni Msimamizi wa Kitengo cha Mauzo, Nouman Vasta. (Picha na Francis Dande).
 Kumtafuta mshindi.
 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wa Reja Reja wa Benki ya I&M, ndabu Lilian Swere, akitangaza majina ya washindi wa droo ya pili ya promosheni ya 'JIDABO na I&MBank.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wa Reja Reja wa Benki ya I&M, Lilian Ndabu , akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza majina ya washindi wa droo ya pili ya promosheni ya 'JIDABO na I&MBank.
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa I&MBank, Emmanuel Kiondo, akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa droo ya pili ya JIDABO na I&MBank.
Msimamizi wa Kitengo cha Mauzo wa I&MBank, Nouman Vasta, akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa droo ya pili ya JIDABO NA I&M BANK.


Dar es Salaam, Tanzania
WASHINDI watano wa droo ya pili ya promosheni ya JIDABO na I&M Benki wamepatikana katika awamu ya pili ya promosheni hiyo iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.

Promosheni hiyo ilizinduliwa wiki ya huduma kwa wateja Duniani inayoazimishwa mwezi Oktoba kila mwaka Benki ya I&M, ilizindua JIDABO na I&M Benki  ambayo mteja mpya anashiriki kwa kufungua Akaunti ya Akiba, Akaunti ya Biashara, Akaunti ya Mshahara na Akaunti ya Mtoto.

lli kushiriki promosheni hiyo mteja anapaswa kufungua Akaunti ya Akiba, Akaunti ya Biashara, Akaunti ya Mshahara au Akaunti ya Mtoto katika tawi Iolote Ia Benki ya I&M katika kipindi cha promosheni. Kwa mteja ambae tayari ana akaunti ya Benki ya I&M anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya Tsh. 200,000I= ikiwa anamiliki Akaunti ya Biashara (Current Account) au Tsh. 100,000I= ikiwa anamiliki akaunti nyingine zinazohusika katika promosheni.

Washindi waliotangazwa leo ni pamoja na Kennedy George, Ayesha Hamza, Naazneen Akil, Leanne Haign na Jameel Zulfikar, akizungumza mara baada ya kuwatangaza washindi hao Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa Benki ya hiyo Lilian Ndabu aliwapongeza na kuwakaribisha Watanzania kujiunga na Benki hiyo,

“Washindi 5 waliopatikana Ieo ni sehemu ya washindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi 3 ya promosheni ya “JIDABO na I&M” na hivo hadi sasa tumeshapata jumla ya washindi 10 na kubakiwa na washindi 5 ambao watapatikana katika droo ya mwezi Desemba.

“Nachukua fursa hii kuwakaribisha Watanzania wote kwa ujumla kuchangamkia fursa hii na kaUngua akaunti katika matawi yetu yanayopatikana mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, A’USha PamOJ'a na Moshi Mkoani Kilimanjaro ili waweze kujidabo na Benki ya I&M na kufanikisha mipango yao mbalimbali iliyobaki katika kuelekea mwisho wa mwaka 2018 na pia kufurahia msimu huu wa sikukuu zaa Krismasi na Mwaka mpya” alisema  Ndabu.

Washindi watano waliopatikana katika droo hiyo ya kwanza ya promosheni ya “JIDABO na I&M Bank” iliyosimamiwa na Bi.Chiku Saleh kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha ni Kwa mujibu wa taratibu za promosheni ya “JIDABO na I&M Bank” washindi hao watano watapata mara mbili ya akiba zilizopo kwenye akaunti zao ambapo kiwango cha juu zaidi kutolewa kwa mteja kitakua Tsh. 5,000,000/=.

No comments:

Post a Comment

Pages