HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2019

Washindi 20 wa NMB MastaBata walamba mkwanja

Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi NMB, Manfred Kayala, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa droo ya nne ya promosheni ya matumizi ya Kadi za NMB MasterCard na Masterpass, ijulikanayo kama NMB MastaBata. (Picha na Francis Dande). 
 
NA MWANDISHI WETU

DROO ya nne ya promosheni ya matumizi ya Kadi za NMB MasterCard na Masterpass, ijulikanayo kama NMB MastaBata, imefanyika mwishoni mwa wiki, ambako wateja 26 wametangazwa washindi wa zawadi ya pesa na simu janja {smartphone}.

NMB MastaBata ni promosheni iliyozinduliwa Desemba 12 mwaka jana, ikilenga kuchagiza matumizi ya malipo kwa kadi za MasterCard na Masterpass, ambako zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 100 zimetengwa, ikiwemo zawadi kuu ya safari ya Dubai iliyolipiwa kila kitu kwa washindi watatu na wenza wao.

Droo ya nne ilifanyika mwishoni wiki katika Tawi la NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambako wateja 20 walijishindia pesa Sh. 100,000 kila mmoja, huku wengine sita wakijinyakulia 'smartphone' aina ya Samsung Galaxy S9+.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania {GBT}, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi NMB, Manfred Kayala, alisema, mwitikio miongoni mwa wateja wa Benki hiyo ni mkubwa na kwamba kwa droo hiyo, wametimiza wiki nne zilizozalisha washindi 80 wa Sh. 100,000 kila mmoja.

Kayala aliwataka wateja wa NMB kuendelea kufanya malipo kwa kutumia NMB MasterCard na NMB Masterpass, ili waweze kushinda mkwanja katika mwezi wa mwisho wa NMB MastaBata, itakayofikia ukomo Februari 14.

"Wito wetu kwa wateja wote ni kuendelea kufanya malipo kwa MasterCard na Masterpass, ili kujishindia fedha, simu na zawadi kuu ya kulipiwa gharama za safari ya kutembelea Dubai kwa washindi watatu na wenza wao watakaowachagua," alisema Kayala.

No comments:

Post a Comment

Pages