HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2019

Bei ya mafuta yawavutia wengi vituo vya Total

Dereva wa bodaboda, Samwel Kisanga, akijaza mafuta kwenye kituo cha Total Oysterbay jijini Dar es Salaam, baada ya kampuni hiyo kutoa punguzo la bei ya mafuta kwa wateja wake katika kusherekea sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’. (Na Mpiga Picha Wetu).
 
NA MWANDISHI WETU

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, jana wamejitokeza na kufurika kwa wingi, katika vituo vya mafuta vya Total, kufuatia punguzo la bei ya mafuta la sh. 70 kwa kila lita, lililotolewa kama zawadi ya sikukuu ya Valentine.

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea baadhi ya vituo, ameshuhudia misusuru ya magari katika vituo vya Total kujaza mafuta na kutokana na punguzo hilo, hata wale madereva ambao huwa wanajaza mafuta kidodo kidogo, juzi walijaza  mengi.

Hali hii imefuatia Kampuni ya Mafuta ya Total, kupunguza bei ya mafuta yake kwa kutoa punguzo la sh. 70 kwa kila lita ya mafuta, kwa muda wa siku tatu, kuanzia Februari 13 hadi 15 katika baadhi ya vituo vyake katika baadhi ya mikoa,Tanzania nzima.

Taarifa hiyo imetolewa na Network Oparations Manager wa vituo vya Total, William Fillet, alisema uamuzi huo wa kupunguza bei ya mafuta katika vituo vya total ni kuwapatia zawadi ya sikukuu ya wapendanao ya Valentine kwa wateja wao, kwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya Valentine kwa Upendo.

Naye Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Total, Marsha Msuya Kileo, amesema sambamba na punguzo hilo la bei katika mafuta, pia wateja wote wa kike, watakao nunua chochote kwenye maduka ya Bonjur, yaliyoko kila kituo cha Total, watapatiwa zawadi ya maua ya Valentine kuonyesha upendo.

Marsha amesema, punguzo hilo, lenye kauli mbiu ya “Fill Up With Love”, yaani jaza mafuta kwa mapenzi na amewakumbusha watanzania, kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha Total, haujazi mafuta tuu, unajaza pua mafuta ya Total Excellium.

Alisema, ni mafuta yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo, kwa kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo, yakiboresha injini ya gari yako.

Jumla ya vituo 16 vya mafuta vya Total viliteuliwa  kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Pages