HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2019

MHE KANYASU AOMBA UMEME WA REA GEITA MJINI

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika jimbo la  Geita mjini kutokana na sababu kuwa  Geita mjini, mjini ni kata mbili tu ikiwemo Kalangalala, Bombambili na maeneo yote yaliyobaki ni vijiji.
Pia, Mhe.Kanyasu amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya  yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa mwaka jana, kijiji kimoja  tu katika jimbo hilo ndo kimenufaika na mradi huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge huyo wakati wa uzinduzi wa umeme wa REA uliofanyika katika kijiji cha ibanda katika wilaya ya Geita mkoani Geita, eneo ambalo  linalohesabika kuwa ni mtaa.
Akizungumza kabla ya kuzindua umeme huo, Dkt.Meldard Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita mjini kuchelewa kupata umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni  mjini na mjini hakuna  vijiji bali kuna mitaa.
"Sisi tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Mhe. Kanyasu ndo kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa bali ni vijiji" Amesisitiza Waziri Kalemani
Hata hivyo, Waziri Kalemani amemhakikishia Mbunge wa Geita mjini kuwa jumla ya vijiji 42 tayari vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani amewaagiza  Wakandarasi na Wataalamu wote kuwa hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba wahakikishe kila mhitaji anaunganishiwa umeme haraka iwezekanavyo.
Aidha, Waziri Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO

No comments:

Post a Comment

Pages