HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 24, 2019

STARS YAICHAPA UGANDA 3-0 NA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA (AFCON 2019)


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars imeshinda 3-0 na kufuzu AFCON 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mechi kati Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Machi 24, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Taifa Stars ilishinda 3-0.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezana na Rais wa TFF,  Wallace Karia baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mechi kati Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salam, Machi 24, 2019.  Taifa Stars ilishinda 3-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa timu ya taifa ya Uganda. (Picha na Said Powa).
 Simon Msuva akishangilia na John Bocco.
 Simon Msuva akishangilia na John Bocco.
 Furaha ya kupata goli.









YAMETIMIA TANZANIA YAFUZU MICHUANO YA AFCON
*Ni baada ya kuifunga Uganda the Craines magoli 3-0

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda  'The Crane' magoli matatu kwa sifuri.

Mechi hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imechezwa katika Uwanja wa Taifa leo (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.

Taifa Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.

Magoli ya  Simon Msuva, Erasto Nyoni na Agrey Morris yalichangia kuivusha Taifa Stars, ambapoMsuva alianza kwa kuipatia gori timu ya Taifa ya Tanzania dakika ya 20 baada ya mechi hiyo kuanza, Nyoni aliipatia Taifa Stars goli la pili dakika ya 50 na dakika sita baadae Moris aliipatia timu ya Taifa goli la tatu.

Kufuatia ushindi huo wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 kutoka kwaKamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na wachezaji hao jana wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao, Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala yeye aliwaahidi kuwapeleka katika mbuga yoyote ya wanyama watakayoichagua kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 24, 2019.

No comments:

Post a Comment

Pages