HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

Awamu ya pili uhakiki wa Jumuiya za Kijamii, Taasisi za Kidini kuanza Juni 23

Na Mwandishi Wetu, MOHA

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini, itaanza kufanya uhakiki wa jumuiya na taasisi hizo kuanzia Juni 23 hadi Julai 2, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alisema uhakiki huo awamu ya pili utaanza Juni 23 hadi Julai 2, katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Manyara.

Meja Jenerali Kingu alisema uhakiki utafanyika kwenye Kituo cha Uhakiki cha iliyokuwa ofisi ya zamani ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni.

Alisema wakati wa uhakiki, jumuiya na taasisi zinapaswa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kikiwemo cheti cha usajili na kivuli cha cheti hicho, stakabadhi ya mwisho ya malipo ya ada iliyolipwa hivi karibuni pamoja na katika ya jumuiya, taasisi husika iliyopitishwa na Msajili.

Nyaraka nyingine nib aria inayothibitisha uwepowa jumuiya, taasisi husika kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa, kata mahali ilipo ofisi ya jumuiya ama taasisi, taarifa za Mkutano Mkuu wa Mwaka pamoja na taarifa ya fedha ya mwaka .

“Fumu ya uhakiki inapatikana kwenye tovuti ya Wizara sambamba na kwenye kituo cha uhakiki, taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo husika zitalazimika kwenda Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma ili kuhakikiwa.

“Na kama zitashindwa kufanya uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye orodha ya Msajili, pia taasisi na jumuiya ambazo hazijasajiliwa zinatakiwa kufika wakati wa uhakiki ili kupewa utaratibu wa kupata usajili,” alisema Meja Jenerali Kingu.

Alifafanua kuwa, malipo ya ada yatafanyika wakati wa uhakiki kupitia mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya kielektroniki (Governmment Electronic Payment Gateway System).

No comments:

Post a Comment

Pages