HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI JIJINI MBEYA WAJIUNGA NA UMOJA WA KITAIFA

 Mwenyekiti wa Soko la Soweto jijini Mbeya, Fredy Mwakongano, akizungumza na Wanawake wafanyabiashara kutoka jijini Dar es Salaam waliofika katika soko hilo juzi kwa ziara ya mafuzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa Kitaifa. Kushoto ni Katibu wa Soko hilo, Atu Mwinuka.
 Mwenyekiti wa muda wa umoja huo Kitaifa kutoka  shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) Betty Mtewele akizungumza.
 Uhamasishaji ukifanyika katika Soko la Soweto
 Uhamasishaji ukiendelea
 Wafanyabiashara wa Soko la Igawilo wakipiga makofi kufurahia umoja huo
 Mfanyabiashara Fatna Konzo akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyopata baada ya kujiunga na EfG
 Ofisa Tathmini na ufuatiliaji wa EfG, Samora Julus akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Igawilo
 Maswali yakiulizwa
 Mfanyabiashara Joanitha Katunzi kutoka Dar es Salaam akihamasisha.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Soweto, Tumaini Kalinga akizunguka na wafanyabiashara wa Soko la Igawilo.
 Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Igawilo.
 Mwanasheria wa EfG, Mussa Mlawa, akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Igawilo.
 Wafanyabiasha wa Soko la Ilomba wakiwa kwenye mkutano wa uhamasishaji.
 Ofisa Tathmini na ufuatiliaji wa EfG, Samora Julus akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Ilomba.
 Mwenyekiti wa Soko la Mabatini Musimu Kipande akizungumza.
 Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Mabatini.
Wafanyabiasha kutoka Dar es Salaam wakiwa na mifuko maalumu waliobebea nyaraka za uhamasishaji.
Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Ilomba.


Na Dotto Mwaibale, Mbeya

WANAWAKE Wafanyabiashara  5000 katika masoko jijini Mbeya wamejiunga na Umoja wa Wanawake Sokoni wa Kitaifa.

Akizungumza jijini Mbeya jana katika ziara ya mafunzo kwa wanawake hao Mwenyekiti wa muda wa umoja huo kitaifa kutoka  shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) Betty Mtewele alisema wamepata mafanikio makubwa baada ya wanawake wafanyabiashara masokoni jijini Mbeya kuhamasika na kujiunga na umoja huo. 

Alisema mafunzo hayo ni utekelezaji wa mikakati na shughuli za programu ya Mwanamke sokoni wa kitaifa ambao umeratibiwa na hilo lenye dhima ya kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi nchini Tanzania hususani kwa wanawake.

" Dhima ya shirika letu ni kuinua sekta hiyo hususani wanawake kwa kuwapunguzia umaskini kwa njia ya kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria, kuwawezesha kuwepo kwa fursa sawa za kibiashara kwa wanawake na wanaume pàmoja na kuwashawishi utungaji wa sera zinazoinua wanawake na kujenga uwezo sawa kwa wanawake na wanaume 

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Penina Leveta alisema EfG ilifanya utafiti mwaka 2009 katika masoko 18 ya jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza mradi wa Sauti ya Mwanamke sokoni unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza ambao ulibainisha sekta isiyorasmi kama chanzo kikuu cha ajira kwa wanawake maskini na ambao hawakusoma nchini Tanzania. 

Alisema ilikadiriwa kuwa asilimia 43 ya wanawake Tanzania wanapata kipato chao kutoka sekta isiyo rasmi hata hivyo ni kwa nadra sana wameshirikishwa katika kufanya maamuzi na kuingizwa katika kamati za masoko, jambo ambalo linadhihirisha kukosa udhibiti juu ya mazingira ya biashara zao na kuwazuia kufanya mabadiliko muhimu ambapo kati ya viongozi 89 wa kamati za masoko wanawake walikuwa ni 14 tu.

Alisema kwa jijini Mbeya wamefanikiwa kuwahamasisha wanawake wafanyabiashra kujiunga na umoja huo katika masoko ya Igawilo, Ilomba, Soweto, Mabatini, Uhindini, Soko Matola, Nzovwe na Ikuti Iyunga.

" Shirika letu lilianzia kufanya kazi ya mradi wa Sauti ya Mwanamke Sokoni jijini Dar es Salaam katika masoko ya Wilaya ya Ilala na Temeke na kuendelea hadi mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya, Lindi, Mtwara na Shinyanga. alisema Leveta.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Soweto, Tumaini Kalinga alisema mafunzo waliyopata kutoka EfG yamewasaidia ambapo wamefanikiwa kuanzisha vikundi vya Vicoba tisa na wanamtaji wa sh.milioni 500, wamenunua bajaj na kiwanja ambacho wanatarajia kujenga hoteli kama chanzo kingine cha mapato yao ambapo katika hatua nyingine amemuomba Naibu Spika Tulia Ackson kuwa mlezi wa umoja wao huo.

No comments:

Post a Comment

Pages