HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 20, 2019

Amani waomba utafiti wa Msambu

Mwenyekiti wa Kijiji cha Shebomeza, Hamisi Barua (kushoto), akiwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Amani, Hadija Nassoro, alizungumza na waandishi wa habari wilayani Muheza mkoani Tanga akizungumzia changamoto ya bei ya zao la Msambu.



NA SULEIMAN MSUYA
SERIKALI imeombwa kufanya utafiti wa zao la Msambu ambalo linapatikana katika Hifadhi ya Mazingira Asili Amani kata ya Amani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Ombi hilo limetolewa na viongozi wa Kijiji cha Shebomeza, kata ya Amani wilaya ya Muheza mkoani Tanga wakati wakizungumza na Habari Mseto Blog hivi karibuni.
Akizungumzia zao hilo Mtendaji wa Kijiji cha Shebomeza, Macheal Siafu alisema zao hilo ambalo linatajwa kupatikana Amani pekee halijanufaisha wananchi hivyo waanamini utafiti ukifanyika bei yake itaongezeka.
Siafu alisema zipo kampuni zinafika kikijiji hapo na kununua Msambu lakini kwa uchunguzi wao wa kawaida wanahisi kuwa bei ambayo inatolewa haiendani na soko la dunia.
“Tunaomba Serikali ilete watafiti waweze kufanya utafiti ili zao hili liweze kujulikana thamani yake halisi ambayo itaondoa hofu walionayo wakulima wanaojihusisha na kilimo hicho,”alisema.
Alisema taarifa walizonazo ni kwamba zao hilo linalopatikana Amani pekee, linatoa mafuta ambayo yanatumika kwa chakula na kutengeneza vanilla.
Siafu alisema zipo taarifa kuwa wapo wanunuzi wanatoka kutoa shilingi 1,500 kwa kilo ila wapo viongozi wengine wanalazimisha iiuzwe shilingi 600 hadi 800.
Alisema zao hilo linakubali katika Ukanda wote wa Hifadhi ya Amani hivyo kukiwa na mpango madhubuti wa kusimamia zao hilo litaongeza mapato ya kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na nchi kwa ujumla.
Mtendaji huyo alisisitiza kuwa mazao ambayo hayajulikani yamekuwa na uhitaji mkubwa hivyo ni wakati muafaka kufanyika kwa tafiti ambazo zitasaidia nchi kuongeza kipato.
Ofisa Mtendaji Kata ya Amani, Hadija Nassoro alisema iwapo jitihada zitaelekezwa katika kukuza na kuongeza thamani ya zao hilo wananchi wajipatia kipato na kufanya shughuli za maendeleo.
Nassoro alisema wananchi wake wamekuwa wakijisghulisha na shughuli za maendeleo lakini wakati mwingine wanakatishwa tama kutokana na bei za mazao yao.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Amani, Bob Matunda alisema zao la Msambu limekuwa na mchango mzuri katika uchumi wa wananchi wa Amani na kwamba utafiti ni muhimu ili kujua thamani ya zao hilo adimu.
Tafiti zinaonesha kuwa Msambu unapatikana hapa Amani pekee naamini tafiti zinahitajika kufanyika ili kujua thamani yake kwani inaweza kuongeza thamani ya wakulima.

No comments:

Post a Comment

Pages